CBC Grade 9 KJSEA Kiswahili Practice Exam · Question 13
Kulingana na aya ya kwanza, huduma katika asasi za kijamii:
From Test 84 — Kiswahili Paper 1 (KJSEA) · 1 mark · Topic: Kusoma, Kusoma kwa Ufahamu
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali kuanzia la 13 hadi la 17.
Huduma katika asasi za kijamii ni muhimu. Asasi hizi huwa na majukumu kwa wanajamii wote. Asasi hizi hutofautiana kutegemea na majukumu yake. Baadhi ya asasi hizi ni kama vile hospitali, mahakama, familia, shule na pia vituo vya usalama. Katika familia, baadhi ya wazazi hawana uwezo wa kuwapa wanao elimu kutokana na umaskini na changamoto nyingine za kimaisha. Kutokana na changamoto kama hizi, asasi nyingine huingilia kati na kuokoa jahazi.
Raia wanapotoa huduma hawapaswi kumbagua yeyote kwa sababu ya dini, kabila, tabaka, maumbile au kiwango cha elimu ya mtu. Ieleweke kuwa hakuna aliye bora zaidi kuliko mwenzake. Ni kinyume cha sheria kwa raia kuzunguka mbuyu ndipo apate huduma anayohitaji. Yeyote anayedai hongo ni kupe anayenyonya damu ya wasio na hatia. Watu wenye hulka hiyo ni adui wa maendeleo katika jamii. Ikiwa mtu anahitaji mapato zaidi, basi afanye bidii katika kazi yake, apandishwe cheo au aanzishe mradi utakaompa hela za ziada. Hakika, mchumi haozi.
Huduma kwenye asasi hizi huhitaji uaminifu, ujanja hauna nafasi. Mbali na hilo, tekeleza majukumu kwa hiari, njia nzuri inayokubalika na kila mmoja. Aidha kumbuka kuwa umoja wetu ni nguvu zetu. Tunaposhirikiana katika utoaji huduma, migogoro hupungua na mshikamano hushamiri siku zote. Mtenda haki hujitendea yeye na nafsiye pamoja na jamii kwa ujumla.

13. Kulingana na aya ya kwanza, huduma katika asasi za kijamii:
- AA. hazifanani
- BB. hugongana
- CC. haziathiri wanajamii
- DD. hufanana
Answer
A. A. hazifanani
Jibu sahihi: A. hazifanani.
More Grade 9 Kiswahili questions from this test
- "Katika familia baadhi ya wazazi hawana uwezo wa kuwapa wanao elimu kutokana na changamoto za umaskini na nyingine za…Question 14
- Aya ya pili inasisitiza jambo gani katika utoaji wa huduma?Question 15
- 'Yeyote anayedai hongo ni kupe anayenyonya damu ya wasio na hatia.' Kauli hii imetumia mbinu gani ya lugha?Question 16
- Mambo yafuatayo yanaweza kufanywa katika utoaji wa huduma katika asasi za kijamii isipokuwa:Question 17
- Kulingana na jedwali hili, ni mchezo upi ambao shule tatu zilipata kushiriki isipokuwa shule moja tu?Question 18
- Neno 'championi' limetumiwa katika kifungu. Kisawe chake si:Question 19