naQonda

CBC Grade 9 KJSEA Kiswahili Practice Exam · Question 7

Udugu ni mojawapo ya maadili yanayochangia mshikamano wa kitaifa. Chagua jibu linaloonyesha udugu wa Sungura katika kifungu:

From Test 84 — Kiswahili Paper 1 (KJSEA) · 1 mark · Topic: Kusoma, Kusoma kwa Ufahamu

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali kuanzia la 7 hadi la 12.
Siku moja, Sungura aliondoka nyumbani kwenda kutafuta chakula msituni. Aliona mbuyu mkubwa sana. Alipoyatupa macho yake juu aliuona mzinga wa asali. Aliamua kurudi zake nyumbani ili awaite wenzake waje kuila asali hiyo. Sungura alielewa kuwa ndugu ni kufaana si kufanana.

Alibisha mlango wa Panya buku naye akamkaribisha kwa moyo mkunjufu. "Baba yangu ameaga dunia na kuniachia mzinga wa asali. Twende tukale asali hiyo." Baada ya maelezo ya kina, Panya buku akaridhia. Wote wakaondoka kuelekea mwituni.

Wote waliupanda mti wakiwa na mienge ya moto waliyoitumia kuwafukuzia nyuki mzingani. Nyuki walitoroka wakapata nafasi ya kuila asali hiyo. Ghafla Simba akatokea chini ya ule mbuyu. Alipoangalia juu aliona asali ikirinwa. "Nyinyi ni nani?" Simba aliuliza. Sungura akamwambia Panya buku, "Nyamaza, ana kichaa mzee yule!" Simba akarudia tena swali lile lile. Panya buku akashikwa na wahaka aliposikia mngurumo wa Simba akasema, "Sisi hapa!" Sungura akamwambia Buku, "Nitwae mimi unitie ndani ya mwenge, mwambie mzee Simba jitenge niutupe mwenge nami naja." Buku akafanya hivyo, ulipoanguka chini, Sungura akafyatuka kama mshale akajiendea zake.

Baada ya dakika chache, Simba akamwambia Buku, “Haya shuka basi”. Buku akashuka kwa hofu na wasiwasi mkubwa. Alipofika chini, Simba alimkamata na kumuuliza, "Ulikuwa wewe na nani?" Akamwambia, "Mimi na Sungura." Kwa hasira Simba alimla papo hapo. Akaapa kuwa atamtafuta Sungura na kumwadhibu. "Sungura hajui shida nilizopitia kuwatunza nyuki wangu. Atakiona cha mtema kuni." Mke wake Simba alifika papo hapo. Kwa mshangao mkubwa akasema, "Lo! Kweli kitanda usichokilalia hujui kunguni wake."

7. Udugu ni mojawapo ya maadili yanayochangia mshikamano wa kitaifa. Chagua jibu linaloonyesha udugu wa Sungura katika kifungu:

  1. AA. Sungura kuingia ndani ya mwenge
  2. BB. Panya buku kushirikiana na Sungura kuiba asali ya Simba
  3. CC. Sungura kumwambia Buku kuwa Simba ana kichaa
  4. DD. Sungura kuwaita wenzake wale asali aliyopata mwituni

Answer

D. D. Sungura kuwaita wenzake wale asali aliyopata mwituni

Jibu sahihi: D. Sungura kuwaita wenzake wale asali aliyopata mwituni.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 9 Kiswahili questions from this test