CBC Grade 8 Kiswahili Mid Term 1 Exam 2025 · Question 10
“Kuwa na nia pekee hakutoshi kumletea mtu mafanikio. Azma hiyo inapaswa kuandamana na uwajibikaji. Mtu akilaza damu huwa muhali kupata mafanikio maishani.”…
From Kiswahili — Mid Term Assessment, Term 1 2025 (Set 5) · 2 marks · Topic: Kusoma, Ufupisho
UFUPISHO
Soma kifungu hiki kisha ujibu swali la 9 hadi 12.
Hakuna mtu ambaye hawezi kufanikiwa maishani. Kila mmoja akiwa na nia thabiti na kufuatilia ndoto zake kikamilifu ataweza kuzitimiza kwa wakati wake. Jambo la kusikitisha ni kuwa watu wengi, wazee kwa vijana, wake kwa waume, hukata tamaa, yaani kupoteza matumaini mafanikio yao yanapokawia. Wengine nao husikiliza akina pangu pakavu tia mchuzi ambao huwaonyesha kwamba kung’ang’ania mafanikio ni sawa na kufukuza upepo.
Kuwa na nia pekee hakutoshi kumletea mtu mafanikio. Azma hiyo inapaswa kuandamana na uwajibikaji. Mtu akilaza damu huwa muhali kupata mafanikio maishani. Lazima afanye bidii mithili ya mchwa huku akielewa kuwa mtaka cha mvunguni sharti ainame. Pia azibe maskio yake ili asiwasikilize wale wanaojaribu kumvunja moyo, nia yao huwa kuzuilia mafanikio yake.
Kuanzia leo, usiwe mtu anayechukulia kuwa mafanikio maishani ni ya watu wachache. Siku zote usadiki kuwa u miongoni mwa waja ambao Mwenyezi Mungu amepangia ufanisi. Ujitahidi kwa vyovyote vile huku ukielewa kuwa penye nia pana njia.
10. “Kuwa na nia pekee hakutoshi kumletea mtu mafanikio. Azma hiyo inapaswa kuandamana na uwajibikaji. Mtu akilaza damu huwa muhali kupata mafanikio maishani.” Kifungu hiki kimetumika katika aya ya pili. Kifupishe kwa maneno yasiyozidi manane. (alama 2)
Answer
Mafanikio yanahitaji nia pamoja na uwajibikaji.
Maneno manane au machache.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 8 Kiswahili questions from this test
- Fupisha aya ya mwisho kwa sentensi moja. (alama 1)Question 11
- Andika kichwa kifaacho zaidi kwa kifungu hiki. (alama 1)Question 12
- SEHEMU 3: LUGHA 18. Pigia mstari vivumishi vya sifa kati ya hizi. Safi, gumu, yule, hicho, hapa, yangu, kwao, vinne,…Question 18
- Sentensi ‘Matano atazifua nguo za wanuna wake’ iko katika wakati ujao. Iandike upya sentensi hiyo katika hali timilifu.Question 19
- Tumia viambishi vifaavyo zaidi kujaza nafasi katika sentensi hii. Michezo aliyoshiriki …me…boresha afya yake.Question 20
- Tambulisha kitenzi kikuu katika sentensi ifuatayo. Ayub hajawahi kulitembelea jiji kuu nchini.Question 21