naQonda

CBC Grade 8 Kiswahili Exam Term 2 2026 · Question 11

(c) Fafanua masuala mawili yaliyoangaziwa katika sehemu hii ya novela. (Alama 4)

From Kiswahili — Term 2 Assessment May 2026 (Set 1) · 4 marks · Topic: Kusoma, Novela

Soma sehemu ifuatayo ya novela kisha ujibu maswali.

Jioni hiyo, Samira alipotoka shuleni, alifululiza moja kwa moja hadi nyumbani. Moyo wake ulijawa furaha furifuri. Alitaka kumweleza mama yake habari njema kutoka shuleni.

“Mama! Mama… Shikamoo!” alisema kwa sauti iliyojawa na bashasha.

Hata hivyo, alijibiwa na mwangwi. Alishtuka ghafla. Moyo ulianza kumdunda dududu! Alikimbilia kwenye kitanda cha mama yake akampata amelala pale si hayati si mamati.

Alimgusa akagundua kuwa mwili wake haukuwa baridi kwa hivyo alikuwa hai. Alitoa simu akabofya nambari za dharura. Simu ikapokelewa upande wa pili. Kwa ukakamavu, alieleza hali ya mamake kisha akaweka simu chini.

Muda mfupi baadaye, alisikia king’ora kilichoashiria kufika kwa ambulance kutoka hospitali ya Okoa Maisha. Himahima wahudumu wale walitoa machela wakaingia chumbani alimokuwa mgonjwa.

Kwa bahati nzuri, Samira alikuwa ameanza kumfanyia huduma ya kwanza.

Ndani ya ambulensi mawazo yalimvamia Samira jinsi nzige washambuliavyo shamba la mihogo.

Aliziona dhiki zilizomshambulia mama yake tangu marehemu baba yake alipoaga dunia. Hali ilizidi kuwa mbaya ami zake walipowanyang’anya kila kitu kwa sababu mama yake alikiuka utamaduni wa kurithiwa na mmoja wao.

Tangu hapo, mamake Samira alikuwa hajiwezi kwa huzuni na mawazo mazito.

Mawazo yake yalikatizwa ambulensi ilipotia nanga hospitalini.

“Tufanye haraka ili tuyaokoe maisha ya mgonjwa kwani hamjui chelewa chelewa utapata mwana si wako?” aliuliza muuguzi mkuu.

(c) Fafanua masuala mawili yaliyoangaziwa katika sehemu hii ya novela. (Alama 4)

Answer

Dhuluma dhidi ya wajane: ami zake Samira waliwanyang'anya kila kitu baada ya mama yake kukataa kurithiwa. Huduma ya kwanza na uwajibikaji: Samira alipiga nambari ya dharura kwa ukakamavu na kumfanyia mama yake huduma ya kwanza.

Suala ni jambo linalozungumziwa na mwandishi. Katika sehemu hii kuna dhuluma kwa wajane, mila ya kurithi wajane, ugonjwa unaotokana na huzuni na mawazo mazito, na huduma ya kwanza na ya dharura.

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 8 Kiswahili questions from this test