CBC Grade 8 Kiswahili Exam Term 2 2026 · Question 15
(c) Jadili maudhui mawili yanayojitokeza kupitia mazungumzo ya wahusika katika sehemu hii ya tamthilia. (Alama 4)
From Kiswahili — Term 2 Assessment May 2026 (Set 1) · 4 marks · Topic: Kusoma, Tamthilia
Soma sehemu ifuatayo ya tamthilia kisha ujibu maswali.
(Sila na Mogomba wamekaa katika meza moja iliyo karibu na dirisha. Mhudumu anafika walipo. Ni binti mwenye umri wa takriban miaka kumi na minane.)
Mhudumu: Hamjambo ndugu zangu? Mngependa niwauzie nini?
Wote: Hatujambo.
Sila: Naomba unisaidie ugali kwa mchicha. Tafadhali utie chumvi kidogo sana.
Mogomba: Nami utanisaidia chai kwa chapati. Sukari isiwe imekolea sana ili isije kuniathiri.
Mhudumu: (Akiandika kwenye kijikaratasi) Sawa. Mtaniruhusu niwashughulikie order yenu. Mkihitaji kitu kingine mtaniambia.
Wote: Asante.
(Mhudumu anaondoka)
Sila: Lakini mbona binti huyu mrembo kama malaika anafanya kazi hii? Kazi ya hoteli ni ya watu wa hadhi ya chini.
Mogomba: Aka! Usiseme hivyo rafiki yangu. Kumbuka kazi mbi si mchezo mwema. Sisi hapa tulipo hatuna kazi wala bazi. Tumeshindia nini binti huyu?
Sila: (Akitabasamu) Hapo umetoa pointi muhimu. Labda kubagua kazi ndiko kunakotufanya tule mwata kila siku.
Mogomba: Jana mambo yalikuwa vipi? Ulisema ungehudhuria mahojiano ya kazi ya uhasibu.
Sila: (Akionyesha wasiwasi) Nilifika kama nilivyoahidiwa. Japo nilihojiwa sijui kama nitapata nafasi. Unajua Kenya ni nchi ya kitu kidogo.
Mogomba: Hilo ndilo tatizo la nchi hii. Nafasi inamwacha aliyehitimu na kumwendea asiye na ujuzi wowote.
(Chakula chao kinaletwa. Wanaanza kula.)
(c) Jadili maudhui mawili yanayojitokeza kupitia mazungumzo ya wahusika katika sehemu hii ya tamthilia. (Alama 4)
Answer
Ukosefu wa ajira: Mogomba anasema "Sisi hapa tulipo hatuna kazi wala bazi." Ufisadi (hongo): Sila anasema "Kenya ni nchi ya kitu kidogo" na nafasi za kazi huwaendea wasiohitimu.
Maudhui ni mafunzo au masuala makuu yanayojadiliwa. Wahusika wanazungumzia ukosefu wa kazi, kubagua au kudharau kazi, ufisadi katika kuajiri, na lishe bora inayolinda afya.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 8 Kiswahili questions from this test
- (d) Wahusika katika sehemu hii ya tamthilia wana uhusiano gani? (Alama 2)Question 16
- (e) Taja kipengele kimoja cha lugha kilichotumiwa katika sehemu hii ya tamthilia. (Alama 2)Question 17
- SEHEMU YA A: KUANDIKA (Alama 15) Matokeo ya mtihani yametolewa. Rafiki yako ameibuka miongoni mwa wanafunzi bora…Question 1
- SEHEMU B (Alama 35) ZOEZI II: FASIHI SIMULIZI (Alama 15) (a) Andika sifa tatu za fasihi simulizi. (Alama 3)Question 2
- (b) Fafanua manufaa mawili ya fasihi katika jamii. (Alama 2)Question 3
- (a) Hadithi hii ni ya aina gani? (Alama 1)Question 4