naQonda

CBC Grade 8 Kiswahili Exam Term 2 2026 · Question 17

(e) Taja kipengele kimoja cha lugha kilichotumiwa katika sehemu hii ya tamthilia. (Alama 2)

From Kiswahili — Term 2 Assessment May 2026 (Set 1) · 2 marks · Topic: Kusoma, Tamthilia

Soma sehemu ifuatayo ya tamthilia kisha ujibu maswali.

(Sila na Mogomba wamekaa katika meza moja iliyo karibu na dirisha. Mhudumu anafika walipo. Ni binti mwenye umri wa takriban miaka kumi na minane.)

Mhudumu: Hamjambo ndugu zangu? Mngependa niwauzie nini?

Wote: Hatujambo.

Sila: Naomba unisaidie ugali kwa mchicha. Tafadhali utie chumvi kidogo sana.

Mogomba: Nami utanisaidia chai kwa chapati. Sukari isiwe imekolea sana ili isije kuniathiri.

Mhudumu: (Akiandika kwenye kijikaratasi) Sawa. Mtaniruhusu niwashughulikie order yenu. Mkihitaji kitu kingine mtaniambia.

Wote: Asante.

(Mhudumu anaondoka)

Sila: Lakini mbona binti huyu mrembo kama malaika anafanya kazi hii? Kazi ya hoteli ni ya watu wa hadhi ya chini.

Mogomba: Aka! Usiseme hivyo rafiki yangu. Kumbuka kazi mbi si mchezo mwema. Sisi hapa tulipo hatuna kazi wala bazi. Tumeshindia nini binti huyu?

Sila: (Akitabasamu) Hapo umetoa pointi muhimu. Labda kubagua kazi ndiko kunakotufanya tule mwata kila siku.

Mogomba: Jana mambo yalikuwa vipi? Ulisema ungehudhuria mahojiano ya kazi ya uhasibu.

Sila: (Akionyesha wasiwasi) Nilifika kama nilivyoahidiwa. Japo nilihojiwa sijui kama nitapata nafasi. Unajua Kenya ni nchi ya kitu kidogo.

Mogomba: Hilo ndilo tatizo la nchi hii. Nafasi inamwacha aliyehitimu na kumwendea asiye na ujuzi wowote.

(Chakula chao kinaletwa. Wanaanza kula.)

(e) Taja kipengele kimoja cha lugha kilichotumiwa katika sehemu hii ya tamthilia. (Alama 2)

Answer

Tashbihi: "binti huyu mrembo kama malaika".

Tashbihi ni ulinganisho unaotumia 'kama': uzuri wa binti unalinganishwa na wa malaika. Vipengele vingine ni methali (kazi mbi si mchezo mwema), nahau (hatuna kazi wala bazi), kuchanganya ndimi (order, pointi), swali la balagha na nidaa (Aka!).

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 8 Kiswahili questions from this test