CBC Grade 8 Kiswahili Exam Term 2 2026 · Question 5
(b) Taja sifa mbili zinazomtambulisha Lwanda kama jagina katika hadithi hii. (Alama 2)
From Kiswahili — Term 2 Assessment May 2026 (Set 1) · 2 marks · Topic: Kusoma, Fasihi Simulizi
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
Lwanda Magere alikuwa shujaa wa Waluo. Alikuwa wa ajabu sana. Alikuwa mwenye nguvu na uwezo wa kushangaza uliomwezesha kufanya jambo ambalo mtu wa kawaida au hata watu kadhaa wasingemudu kufanya.
Majirani wa Waluo, Walang’o walikuwa na mazoea ya kuwaibia ng’ombe. Kila Lwanda alipokabiliana nao aliwashinda vibaya. Walang’o walishangazwa na uwezo wa Lwanda Magere. Walishindwa kuelewa kwa nini alikuwa na mwili uliokuwa mgumu mithili ya jiwe. Kila walipoupiga mkuki haukudhurika. Mikuki yao ilisalimu amri.
Ili kujua asili ya nguvu zake, Walang’o walipanga kumtafutia msichana wao mmoja aliyekuwa hurulaini. Msichana huyo ndiye angewachunguzia siri ya Lwanda ili waitumie kumwangamiza. Lwanda alimwoa binti huyo bila kujua kuwa vyote ving’aavyo si dhahabu.
Mke wa kwanza wa Lwanda hakupendezwa na tabia hiyo. Alishuku kuwa msichana yule alikuwa mtego wa kumnasa Lwanda. Alimhimiza Lwanda amtafute msichana mzuri kutoka jamii yao afunge akidi naye.
Lwanda alikataa katakata kuzingatia waadhi huo.
Siku moja Lwanda aliugua wakati ambapo mkewe wa kwanza alikuwa ameenda shambani kupalilia mimea. Lwanda alipoona maradhi yanamzidia alimwambia mkewe wa pili achanje chale kivuli chake na kumtia dawa.
Mara baada ya kujua siri ya Lwanda msichana yule wa Kilang’o alifurahi sana. Kivuli kinachanjwa chale na mwili wa jitu kutokwa damu? Basi alifunganya virago na kurudi kwao kutoboa siri ya Lwanda.
Siku chache baadaye, Walang’o walianzisha vita dhidi ya Waluo. Lwanda alipopata habari kwamba watu wake wamelemewa alitoka kwenda vitani ambapo aliwafukuzilia mbali Walang’o. Aliwasafirisha wengi jongomeo.
Hata hivyo, Walang’o walikumbuka siri waliyopewa na msichana yule waliyemwoza kwa Lwanda. Walimvizia na kukichoma kivuli chake mkuki na kumwua. Lwanda alipoanguka chini mwili wake ulibadilika ukawa jiwe kubwa.
(b) Taja sifa mbili zinazomtambulisha Lwanda kama jagina katika hadithi hii. (Alama 2)
Answer
Alikuwa na nguvu za ajabu zisizo za kawaida; mwili wake ulikuwa mgumu kama jiwe hivi kwamba mikuki haikumdhuru.
Jagina ni shujaa wa mighani mwenye uwezo usio wa kawaida. Lwanda alikuwa na nguvu za kushangaza, mwili mgumu kama jiwe, nguvu zake zilitokana na kivuli chake, aliwashinda maadui peke yake, na alipokufa aligeuka jiwe.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 8 Kiswahili questions from this test
- (c) Tambulisha shughuli mbili za kiuchumi ambazo jamii ya kifungu hiki ilishiriki. (Alama 2)Question 6
- (d) Fafanua vipengele vitatu vya uwasilishaji ambavyo fanani anapaswa kuzingatia anapowasilisha hadithi hii. (Alama 3)Question 7
- (e) Eleza mafunzo mawili yanayojitokeza katika hadithi hii. (Alama 2)Question 8
- ZOEZI III: NOVELA (Alama 10) (a) Taja aina tatu za mandhari zinazojitokeza katika sehemu hii ya novela. (Alama 3)Question 9
- (b) Kwa nini Samira alifululiza mwendo hadi nyumbani? (Alama 1)Question 10
- (c) Fafanua masuala mawili yaliyoangaziwa katika sehemu hii ya novela. (Alama 4)Question 11