CBC Grade 8 Kiswahili Exam Term 2 2026 · Question 10
(b) Kwa nini Samira alifululiza mwendo hadi nyumbani? (Alama 1)
From Kiswahili — Term 2 Assessment May 2026 (Set 1) · 1 mark · Topic: Kusoma, Novela
Soma sehemu ifuatayo ya novela kisha ujibu maswali.
Jioni hiyo, Samira alipotoka shuleni, alifululiza moja kwa moja hadi nyumbani. Moyo wake ulijawa furaha furifuri. Alitaka kumweleza mama yake habari njema kutoka shuleni.
“Mama! Mama… Shikamoo!” alisema kwa sauti iliyojawa na bashasha.
Hata hivyo, alijibiwa na mwangwi. Alishtuka ghafla. Moyo ulianza kumdunda dududu! Alikimbilia kwenye kitanda cha mama yake akampata amelala pale si hayati si mamati.
Alimgusa akagundua kuwa mwili wake haukuwa baridi kwa hivyo alikuwa hai. Alitoa simu akabofya nambari za dharura. Simu ikapokelewa upande wa pili. Kwa ukakamavu, alieleza hali ya mamake kisha akaweka simu chini.
Muda mfupi baadaye, alisikia king’ora kilichoashiria kufika kwa ambulance kutoka hospitali ya Okoa Maisha. Himahima wahudumu wale walitoa machela wakaingia chumbani alimokuwa mgonjwa.
Kwa bahati nzuri, Samira alikuwa ameanza kumfanyia huduma ya kwanza.
Ndani ya ambulensi mawazo yalimvamia Samira jinsi nzige washambuliavyo shamba la mihogo.
Aliziona dhiki zilizomshambulia mama yake tangu marehemu baba yake alipoaga dunia. Hali ilizidi kuwa mbaya ami zake walipowanyang’anya kila kitu kwa sababu mama yake alikiuka utamaduni wa kurithiwa na mmoja wao.
Tangu hapo, mamake Samira alikuwa hajiwezi kwa huzuni na mawazo mazito.
Mawazo yake yalikatizwa ambulensi ilipotia nanga hospitalini.
“Tufanye haraka ili tuyaokoe maisha ya mgonjwa kwani hamjui chelewa chelewa utapata mwana si wako?” aliuliza muuguzi mkuu.
(b) Kwa nini Samira alifululiza mwendo hadi nyumbani? (Alama 1)
Answer
Alitaka kumweleza mama yake habari njema kutoka shuleni.
Kifungu kinasema moyo wake ulijawa furaha na alitaka kumweleza mama yake habari njema kutoka shuleni.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 8 Kiswahili questions from this test
- (c) Fafanua masuala mawili yaliyoangaziwa katika sehemu hii ya novela. (Alama 4)Question 11
- (d) Huku ukitolea mifano mwafaka, eleza vipengele vitatu vya lugha vilivyotumiwa katika sehemu hii ya novela. (Alama 3)Question 12
- ZOEZI IV: TAMTHILIA (Alama 10) (a) Ni mandhari yapi yanayojitokeza katika sehemu hii ya tamthilia? (Alama 1)Question 13
- (b) Taja sifa mbili zinazoonyesha kuwa kifungu hiki ni mfano wa tamthilia. (Alama 2)Question 14
- (c) Jadili maudhui mawili yanayojitokeza kupitia mazungumzo ya wahusika katika sehemu hii ya tamthilia. (Alama 4)Question 15
- (d) Wahusika katika sehemu hii ya tamthilia wana uhusiano gani? (Alama 2)Question 16