CBC Grade 8 Kiswahili Exam Term 2 2026 · Question 12
(d) Huku ukitolea mifano mwafaka, eleza vipengele vitatu vya lugha vilivyotumiwa katika sehemu hii ya novela. (Alama 3)
From Kiswahili — Term 2 Assessment May 2026 (Set 1) · 3 marks · Topic: Kusoma, Novela
Soma sehemu ifuatayo ya novela kisha ujibu maswali.
Jioni hiyo, Samira alipotoka shuleni, alifululiza moja kwa moja hadi nyumbani. Moyo wake ulijawa furaha furifuri. Alitaka kumweleza mama yake habari njema kutoka shuleni.
“Mama! Mama… Shikamoo!” alisema kwa sauti iliyojawa na bashasha.
Hata hivyo, alijibiwa na mwangwi. Alishtuka ghafla. Moyo ulianza kumdunda dududu! Alikimbilia kwenye kitanda cha mama yake akampata amelala pale si hayati si mamati.
Alimgusa akagundua kuwa mwili wake haukuwa baridi kwa hivyo alikuwa hai. Alitoa simu akabofya nambari za dharura. Simu ikapokelewa upande wa pili. Kwa ukakamavu, alieleza hali ya mamake kisha akaweka simu chini.
Muda mfupi baadaye, alisikia king’ora kilichoashiria kufika kwa ambulance kutoka hospitali ya Okoa Maisha. Himahima wahudumu wale walitoa machela wakaingia chumbani alimokuwa mgonjwa.
Kwa bahati nzuri, Samira alikuwa ameanza kumfanyia huduma ya kwanza.
Ndani ya ambulensi mawazo yalimvamia Samira jinsi nzige washambuliavyo shamba la mihogo.
Aliziona dhiki zilizomshambulia mama yake tangu marehemu baba yake alipoaga dunia. Hali ilizidi kuwa mbaya ami zake walipowanyang’anya kila kitu kwa sababu mama yake alikiuka utamaduni wa kurithiwa na mmoja wao.
Tangu hapo, mamake Samira alikuwa hajiwezi kwa huzuni na mawazo mazito.
Mawazo yake yalikatizwa ambulensi ilipotia nanga hospitalini.
“Tufanye haraka ili tuyaokoe maisha ya mgonjwa kwani hamjui chelewa chelewa utapata mwana si wako?” aliuliza muuguzi mkuu.
(d) Huku ukitolea mifano mwafaka, eleza vipengele vitatu vya lugha vilivyotumiwa katika sehemu hii ya novela. (Alama 3)
Answer
Tanakali za sauti: "Moyo ulianza kumdunda dududu!". Tashbihi: "mawazo yalimvamia Samira jinsi nzige washambuliavyo shamba la mihogo". Methali: "chelewa chelewa utapata mwana si wako".
Vipengele vya lugha ni mbinu zinazopamba maandishi. Hapa kuna tanakali za sauti (dududu, furaha furifuri), tashbihi (jinsi nzige washambuliavyo), methali (chelewa chelewa…), nahau (aliaga dunia, ilipotia nanga), swali la balagha (hamjui …?) na tashihisi (alijibiwa na mwangwi, mawazo yalimvamia).
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 8 Kiswahili questions from this test
- ZOEZI IV: TAMTHILIA (Alama 10) (a) Ni mandhari yapi yanayojitokeza katika sehemu hii ya tamthilia? (Alama 1)Question 13
- (b) Taja sifa mbili zinazoonyesha kuwa kifungu hiki ni mfano wa tamthilia. (Alama 2)Question 14
- (c) Jadili maudhui mawili yanayojitokeza kupitia mazungumzo ya wahusika katika sehemu hii ya tamthilia. (Alama 4)Question 15
- (d) Wahusika katika sehemu hii ya tamthilia wana uhusiano gani? (Alama 2)Question 16
- (e) Taja kipengele kimoja cha lugha kilichotumiwa katika sehemu hii ya tamthilia. (Alama 2)Question 17
- SEHEMU YA A: KUANDIKA (Alama 15) Matokeo ya mtihani yametolewa. Rafiki yako ameibuka miongoni mwa wanafunzi bora…Question 1