CBC Grade 7 Kiswahili Exam Term 1 2026 · Question 4
Umejifunza nini kutokana na kifungu hiki? (1 alama)
From Kiswahili — Term 1 February Assessment 2026 (Set 2) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Hadithi
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali ya 1 hadi 4.
Katika shamba la mkulima mmoja, walikuwemo kondoo na jogoo. Kondoo alipendwa na wanyama wengine humo shambani kutokana na upole, ukarimu na kujali maslahi ya wengine. Jogoo kwa upande mwingine hakuwa na marafiki wengi kutokana na utukutu na majisifu yake. Lililowakera zaidi ni jinsi jogoo alivyofurahia masaibu ya wengine badala ya kuwasikitikia.
Siku moja, jogoo alimsikia mzee mwenye shamba akimwambia mkewe, “Mke wangu, wazazi na ndugu zako wametuma taarifa kwamba watatutembelea juma lijalo. Sitaki wanichukulie kama mwenye mkono birika. Itabidi tumchinje kondoo ili wageni washibe kitoweo.”
Mke alikubaliana naye.
Jogoo alikimbia kwa haraka akatangaza kuwa kondoo angechinjwa wiki ijayo. Hakujali kuwa maneno yake yalimuumiza kondoo na wanyama waliompenda.
Kondoo alimwomba Muumba wake kwa imani kuwa mcha Mungu si mtovu. Siku chache kabla ya wageni kufika, walituma ujumbe kuwa safari imeahirishwa kwa sababu babamkwe wa mwenye shamba alikuwa mgonjwa. Kondoo alinusurika, lakini jogoo aliugua ghafla na kufa.
4. Umejifunza nini kutokana na kifungu hiki? (1 alama)
Answer
Usifurahie shida za wengine; Mungu humlinda mwenye haki.
Jogoo aliyefurahia masaibu ya wengine aliishia kufa; kondoo mpole aliokolewa.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 7 Kiswahili questions from this test
- SEHEMU B: UFAHAMU 5. Jukumu la kudumisha usafi ni la nani? (1 alama)Question 5
- Wakaazi wanaweza kuonyesha uwajibikaji kwa:Question 6
- Taja ugonjwa mmoja unaosababishwa na uchafu. (1 alama)Question 7
- Kisawe cha neno dhati ni nini?Question 8
- Andika habari kuu ya aya ya kwanza kwa sentensi moja. (1 alama)Question 9
- Fupisha ujumbe huu kwa maneno yasiyozidi kumi: “Vijana wakitumia maarifa yao wanaweza kuzalisha bidhaa nchini.”Question 10