naQonda

CBC Grade 7 Kiswahili Exam Term 1 2026 · Question 3

Nini kilimwokoa kondoo? (1 alama)

From Kiswahili — Term 1 February Assessment 2026 (Set 2) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Hadithi

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali ya 1 hadi 4.
Katika shamba la mkulima mmoja, walikuwemo kondoo na jogoo. Kondoo alipendwa na wanyama wengine humo shambani kutokana na upole, ukarimu na kujali maslahi ya wengine. Jogoo kwa upande mwingine hakuwa na marafiki wengi kutokana na utukutu na majisifu yake. Lililowakera zaidi ni jinsi jogoo alivyofurahia masaibu ya wengine badala ya kuwasikitikia.
Siku moja, jogoo alimsikia mzee mwenye shamba akimwambia mkewe, “Mke wangu, wazazi na ndugu zako wametuma taarifa kwamba watatutembelea juma lijalo. Sitaki wanichukulie kama mwenye mkono birika. Itabidi tumchinje kondoo ili wageni washibe kitoweo.”
Mke alikubaliana naye.
Jogoo alikimbia kwa haraka akatangaza kuwa kondoo angechinjwa wiki ijayo. Hakujali kuwa maneno yake yalimuumiza kondoo na wanyama waliompenda.
Kondoo alimwomba Muumba wake kwa imani kuwa mcha Mungu si mtovu. Siku chache kabla ya wageni kufika, walituma ujumbe kuwa safari imeahirishwa kwa sababu babamkwe wa mwenye shamba alikuwa mgonjwa. Kondoo alinusurika, lakini jogoo aliugua ghafla na kufa.

3. Nini kilimwokoa kondoo? (1 alama)

Answer

Wageni waliahirisha safari (baada ya kondoo kumwomba Muumba).

Kondoo aliomba, na wageni wakaahirisha safari kwa sababu babamkwe alikuwa mgonjwa.

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 7 Kiswahili questions from this test