CBC Grade 7 Kiswahili Opener Exam Term 2 2025 · Question 5
Jukumu la kudumisha usafi wa maeneo mbalimbali ni la nani?
From Kiswahili — Term 2 Opener Assessment 2025 (Set 10) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Makala
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali la 5 hadi la 8.
Ingawa serikali za magatuzi mbalimbali zina jukumu kubwa katika kudumisha usafi katika maeneo ya miji, wakazi wa maeneo hayo hawafai kujipakatia mikono huku wakingojea kufanyiwa kila kitu. Lazima wawajibike ipasavyo kwa kuchukua hatua ambazo hazitavuruga mazingira na kuishia kuwa kero na hatari kwao na wenzao.
Mathalani, wakaazi wanaweza kutenga siku katika mwezi ambapo watashiriki kwa pamoja shughuli za kudumisha usafi ikifika siku hiyo, wajitokeze kwa wingi huku wamebeba sepetu, reki, kwanja na vifaa vingine muhimu. Ni muhimu wavalie mavazi yafaayo ili kujikinga dhidi ya athari zitokanazo na uchafu kama vile kudungwa na vitu vyenye kuathiriwa na bakteria katika uchafu.
Usafi wa mazingira ni jambo linalopaswa kuzingatiwa kwa dhati na kila mmoja. Uchafuzi wa mazingira unaofanywa na watu wenye mapuuza unaweza kuwa chanzo cha majuto baadaye.
5) Jukumu la kudumisha usafi wa maeneo mbalimbali ni la nani?
Answer
Ni la serikali za magatuzi na wakazi wa maeneo hayo.
Kifungu kinasema serikali za magatuzi zina jukumu kubwa, lakini wakazi nao lazima wawajibike; aya ya mwisho inasema usafi ni jambo la kila mmoja.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 7 Kiswahili questions from this test
- Wananchi wanawezaje kuonyesha uwajibikaji wao?Question 6
- Watu wanapaswa kuvalia mavazi yafaayo wanaposhiriki shughuli za kunadhifisha mazingira. Taja ugonjwa mmoja unaotokana…Question 7
- Neno sepetu lina maana sawa na beleshi. Kisawe cha neno dhati ni?Question 8
- Andika habari kuu katika aya ya kwanza kwa sentensi moja.Question 9
- Vijana wakitumia maarifa wanayopata katika taasisi za kielimu wanaweza kuunda bidhaa humu humu nchini ili tuache…Question 10
- Andika ujumbe uliokolezwa rangi katika aya ya mwisho kwa sentensi moja. Ujumbe uliokolezwa rangi ni: "Tukiendelea na…Question 11