naQonda

CBC Grade 7 Kiswahili Exam Term 1 2026 · Question 1

Kifungu hiki kimezungumzia kuhusu

From Kiswahili — Term 1 February Assessment 2026 (Set 2) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Makala

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali ya 1 hadi 6.
Watoto wengi siku hizi hutumia muda mwingi kucheza michezo ya mtandaoni kuliko kufanya mambo ya maana kama kujisomea au kusaidia wazazi wao. Wengine huzoea kutumia simu hadi usiku wa manane. Hali hii imewafanya kuwa na uchovu shuleni na kushindwa kufuata mafunzo ipasavyo. Wazazi wengi wameanza kulalamika kuwa watoto wao hawataki kufanya kazi wala kushiriki shughuli za kijamii.
Walimu nao wanasema kuwa baadhi ya wanafunzi hawazingatii somo kwa sababu ya simu na michezo ya kompyuta. Ni vyema wazazi wakachukua jukumu la kuwafunza watoto kutumia teknolojia kwa njia bora. Teknolojia ni nzuri ikiwa inatumika ipasavyo, lakini inapotumika vibaya, huleta madhara makubwa.

1. Kifungu hiki kimezungumzia kuhusu

  1. Aumuhimu wa teknolojia shuleni
  2. Bmatumizi mabaya ya teknolojia kwa watoto
  3. Cwazazi wanaonunua simu
  4. Dmichezo ya watoto shuleni

Answer

B. matumizi mabaya ya teknolojia kwa watoto

Kifungu kinaeleza jinsi watoto wanavyotumia simu na michezo ya mtandaoni vibaya.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 7 Kiswahili questions from this test