CBC Grade 7 Kiswahili Exam Term 1 2026 · Question 5
Sentensi ipi inayoonyesha matokeo ya matumizi mabaya ya teknolojia?
From Kiswahili — Term 1 February Assessment 2026 (Set 2) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Makala
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali ya 1 hadi 6.
Watoto wengi siku hizi hutumia muda mwingi kucheza michezo ya mtandaoni kuliko kufanya mambo ya maana kama kujisomea au kusaidia wazazi wao. Wengine huzoea kutumia simu hadi usiku wa manane. Hali hii imewafanya kuwa na uchovu shuleni na kushindwa kufuata mafunzo ipasavyo. Wazazi wengi wameanza kulalamika kuwa watoto wao hawataki kufanya kazi wala kushiriki shughuli za kijamii.
Walimu nao wanasema kuwa baadhi ya wanafunzi hawazingatii somo kwa sababu ya simu na michezo ya kompyuta. Ni vyema wazazi wakachukua jukumu la kuwafunza watoto kutumia teknolojia kwa njia bora. Teknolojia ni nzuri ikiwa inatumika ipasavyo, lakini inapotumika vibaya, huleta madhara makubwa.
5. Sentensi ipi inayoonyesha matokeo ya matumizi mabaya ya teknolojia?
- AWatoto hujifunza kwa kasi
- BWazazi hujivunia watoto wao
- CWanafunzi hupata usingizi shuleni
- DWanafunzi huandika insha vizuri
Answer
C. Wanafunzi hupata usingizi shuleni
Kutumia simu hadi usiku wa manane huwaletea watoto uchovu shuleni.