CBC Grade 7 Kiswahili Exam Term 1 2026 · Question 6
Mwandishi ametoa wito gani?
From Kiswahili — Term 1 February Assessment 2026 (Set 2) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Makala
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali ya 1 hadi 6.
Watoto wengi siku hizi hutumia muda mwingi kucheza michezo ya mtandaoni kuliko kufanya mambo ya maana kama kujisomea au kusaidia wazazi wao. Wengine huzoea kutumia simu hadi usiku wa manane. Hali hii imewafanya kuwa na uchovu shuleni na kushindwa kufuata mafunzo ipasavyo. Wazazi wengi wameanza kulalamika kuwa watoto wao hawataki kufanya kazi wala kushiriki shughuli za kijamii.
Walimu nao wanasema kuwa baadhi ya wanafunzi hawazingatii somo kwa sababu ya simu na michezo ya kompyuta. Ni vyema wazazi wakachukua jukumu la kuwafunza watoto kutumia teknolojia kwa njia bora. Teknolojia ni nzuri ikiwa inatumika ipasavyo, lakini inapotumika vibaya, huleta madhara makubwa.
6. Mwandishi ametoa wito gani?
- ATeknolojia ifutwe mashuleni
- BWazazi wachukue jukumu la malezi
- CWalimu wawape watoto michezo
- DWatoto waache kutumia simu kabisa
Answer
B. Wazazi wachukue jukumu la malezi
Mwandishi anasema ni vyema wazazi wachukue jukumu la kuwafunza watoto.