CBC Grade 7 Kiswahili Exam Term 1 2026 · Question 3
Wazazi wanafaa kufanya nini kulingana na kifungu?
From Kiswahili — Term 1 February Assessment 2026 (Set 2) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Makala
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali ya 1 hadi 6.
Watoto wengi siku hizi hutumia muda mwingi kucheza michezo ya mtandaoni kuliko kufanya mambo ya maana kama kujisomea au kusaidia wazazi wao. Wengine huzoea kutumia simu hadi usiku wa manane. Hali hii imewafanya kuwa na uchovu shuleni na kushindwa kufuata mafunzo ipasavyo. Wazazi wengi wameanza kulalamika kuwa watoto wao hawataki kufanya kazi wala kushiriki shughuli za kijamii.
Walimu nao wanasema kuwa baadhi ya wanafunzi hawazingatii somo kwa sababu ya simu na michezo ya kompyuta. Ni vyema wazazi wakachukua jukumu la kuwafunza watoto kutumia teknolojia kwa njia bora. Teknolojia ni nzuri ikiwa inatumika ipasavyo, lakini inapotumika vibaya, huleta madhara makubwa.
3. Wazazi wanafaa kufanya nini kulingana na kifungu?
- AKuwanunulia watoto simu zaidi
- BKuwazuia watoto kutumia intaneti
- CKuwafundisha matumizi bora ya teknolojia
- DKuwatuma watoto mashambani
Answer
C. Kuwafundisha matumizi bora ya teknolojia
"Ni vyema wazazi wakachukua jukumu la kuwafunza watoto kutumia teknolojia kwa njia bora."
More Grade 7 Kiswahili questions from this test
- Neno madhara lina maana sawa naQuestion 4
- Sentensi ipi inayoonyesha matokeo ya matumizi mabaya ya teknolojia?Question 5
- Mwandishi ametoa wito gani?Question 6
- Shule ya Mlimani hufanya shughuli hii iliQuestion 7
- Kulingana na kifungu, kazi hizo hufanywaQuestion 8
- Wimbo uliotajwa katika kifungu una maana yaQuestion 9