CBC Grade 7 Kiswahili Exam Term 3 2026 · Question 12
Matukio yafuatayo yalitokea katika kifungu: i. Wanyama kutumia ziwa. ii. Kobe kumkanya Fisi. iii. Simba kuridhia mpango wa Mbweha. iv. Fisi kushikwa na tamaa.…
From Kiswahili Paper 1 — October 2026 Collection · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa kusoma
Zamani, wanyama waliishi katika nchi ya Jijenge. Simba ndiye aliyekuwa mfalme wao. Nchi hii ilibarikiwa kuwa na rasilimali nyingi. Si madini, si mito, si misitu, si milima, si bahari... Hakika nchi hii ilikuwa nchi yenye baraka.
Wanyama waliishi kwa amani na furaha. Hakuna mnyama aliyelala njaa. Kila mmoja alimjali mwenzake. Aidha, wanyama hao walijifunga kibwebwe kuhakikisha kila mmoja ana mahitaji ya kimsingi.
Ziwa lilikuwa mojawapo ya rasilimali muhimu sana. Humo walipatikana mamba, samaki mbalimbali na viboko kadhaa. Wavuvi wengi walimiminika kule kujizolea riziki. Walifahamu wazi kuwa mgaagaa na upwa hali wali mkavu.
Baadhi ya wanyama walitaka kujinufaisha na ziwa hili kuliko wenzao. Maarufu katika kundi hili alikuwa Fisi. Daima hakuridhika. Alianza kuwahangaisha wanyama wengine waliotumia ziwa hilo.
Mzee Kobe alijaribu kumkanya Fisi, lakini hakujali. Mbweha alitaka kumfunza adabu. Alimweleza Simba mpango wa kumzuia Fisi kufanya vitendo vilivyokuwa kinyume cha haki.
Simba aliridhia mpango wa Mbweha. Fisi alitimua mbio hadi ziwani. Alipotazama ziwani, Fisi alimwona Fisi mwingine akijitazama kwenye maji. Maskini! Fisi hakujua kuogelea. Asingelikuwa Kiboko aliyefika majini wakati huo huo, Fisi angekuwa hadithi ya kusimuliwa.

Matukio yafuatayo yalitokea katika kifungu:
i. Wanyama kutumia ziwa.
ii. Kobe kumkanya Fisi.
iii. Simba kuridhia mpango wa Mbweha.
iv. Fisi kushikwa na tamaa.
v. Fisi kuwahangaisha wanyama.
vi. Fisi kunusurika kifo.
Chagua mfuatano sahihi wa matukio hayo.
- Ai, iv, v, ii, iii, vi
- Bi, ii, iii, iv, v, vi
- Ci, vi, v, ii, iii, iv
- Dvi, v, iv, iii, ii, i
Answer
A. i, iv, v, ii, iii, vi
Wanyama walitumia ziwa, Fisi akatamani kujinufaisha na kuwahangaisha, Kobe akamkanya, Simba akakubali mpango wa Mbweha, kisha Fisi akanusurika.
More Grade 7 Kiswahili questions from this test
- Kulingana na aya ya kwanza, ni jambo gani lilikuwa likitendeka zamani?Question 13
- Ni jawabu gani lililo sahihi kwa mujibu wa kifungu?Question 14
- Kifungu hiki kimebainisha kuwa visa vya ubakaji hutokea kwa sababu ya:Question 15
- Neno “kukithiri” limetumika katika kifungu hiki. Maana yake ni:Question 16
- Maana ya nahau “utashi wa moyo” ni:Question 17
- Ni kijana yupi aliyetengeneza bidhaa tatu?Question 18