CBC Grade 6 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 7
Soma ufahamu unaofuata kisha ujibu swali la 7 hadi 11 Taifa la Kenya lina makabila zaidi ya arubaini na matano. Makabila haya yametapakaa katika maeneo…
From Test 16 — Karatasi ya Marudio 2026 · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Kifungu
Soma ufahamu unaofuata kisha ujibu swali la 7 hadi 11
Taifa la Kenya lina makabila zaidi ya arubaini na matano. Makabila haya yametapakaa katika maeneo mbalimbali ya kijografia kama vile mwambao wa pwani, eneo la Mlima Kenya, bonde la ufa, eneo la Ziwa Viktoria pamoja na ukanda wa Magharibi. Vile vile, kuna jamii nyingi ambazo zinapatikana katika eneo la kaskazini. Nyingi kati ya jamii za huko ni za wafugaji wa kuhamahama.
Jamii hizi huwa na utamaduni tofauti ambao hurithi kutoka kizazi kimoja hadi kingine mfano, jinsi ya kuvaa, vyakula mbalimbali, tamaduni na mila kama vile upashaji tohara, sherehe za harusi na hata maombolezo. Vile vile, jamii zina tamaduni ambazo zinashikilia mavazi, shughuli mbalimbali katika maisha yao ya kila siku.
Jamii kama vile ya Wamaasai, inatambulika kwa kufuga mifugo na kuwalisha. Utamaduni wa kuvaa shuka nyekundu na kubeba silaha umeifanya jamii hii kuwa maarufu sana nchini na hata nje ya bara hili. Watalii wengi wanapozuri nchi hii, hutaka sana kujumuika na Wamaasai ili kuburudishwa na nyimbo zao za kitamaduni.
Mbali na hayo, wao huwa na vyakula vyao vya kitamaduni ambavyo ni kama vile maziwa, nyama na hata damu. Utamaduni wao umewatambulisha kote na kuwafanya kuwa maarufu sana. Inasemekana kuwa hii ndio jamii ya pekee ambayo imeshikilia tamaduni zao hasa wakati ambapo jamii nyingi zimeacha tamaduni zao na kukumbatia usasa.
Jamii nyingi za pwani ya Kenya zinatambulika kwa mapishi yao, nyimbo zao, sherehe zao na shughuli zao za kila siku. Uvuvi na utalii huwa maarufu sana katika owani ya Kenya. Vyakula vya kitamaduni kama vile samaki, vitafunio kama kamati, mahamri na kahawa chungu huthaminiwa sana katika sehemu hizo.
Ni muhimu kwa kila mmoja kutambua kuwa ingawa jamii tofauti zina mila zao, mila na tamaduni hizi hazifai kuwa kigezo cha kututenganisha bali kuwa fahari ya kututambulisha na kutuleta pamoja. Tunafaa kujivunia kile ambacho ni kizuri na kinamilikiwa na watu wengine. Vile vile, jamii nyingine zinafaa kuonea fahari tamaduni za jamii tofauti. Huo ndio mshikamano ambao utajenga taifa letu na kuhakikisha kuwa tunasonga mbele.
Tofauti mbalimbali za kitamaduni miongoni mwetu zina jukumu gani?
- AJukumu la kututambulisha kitaifa
- BJukumu la kutuunganisha pamoja
- CJukumu la kuwavutia watalii
- DJukumu la kuonesha tofauti miongoni mwetu
Answer
A. Jukumu la kututambulisha kitaifa
Kifungu kinasema mila na tamaduni ni "fahari ya kututambulisha na kutuleta pamoja," yaani jukumu la kututambulisha kitaifa.
More Grade 6 Kiswahili questions from this test
- Aya ya pili inasema kuwa utamaduni wa jamii moja hupokezwa kwa jamii ijayo kutoka wapi?Question 8
- Ipi kati ya hizi si miongoni mwa mila na utamaduni wa jamii mbalimbali nchini?Question 9
- Ni jamii zipi ambazo zinatambulika kwa utalii na shughuli za uvuvi miongoni mwa hizi?Question 10
- Ni nini maana ya kuonea fahari kama ilivyotumika kwenye kifungu hiki?Question 11
- Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali kutoka 12 hadi 15 Suzana aliwashangaza wengi alipoibuka kuwa mshindi…Question 12
- Kifungu kinasema kuwa jamii iliamini nini kuhusu uwezo na jinsia?Question 13