naQonda

CBC Grade 6 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 12

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali kutoka 12 hadi 15 Suzana aliwashangaza wengi alipoibuka kuwa mshindi katika mashindano ya uchoraji. Wengi…

From Test 16 — Karatasi ya Marudio 2026 · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Hadithi

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali kutoka 12 hadi 15

Suzana aliwashangaza wengi alipoibuka kuwa mshindi katika mashindano ya uchoraji. Wengi walidhani kuwa uchoraji ulikuwa fani ya wavulana. Suzana, binti wa gredi ya sita katika shule ya Chebukaka hakukata tamaa. Alijua kuwa alikuwa na uwezo mkubwa katika bahari ya uchoraji. Alianza kuchora akiwa mdogo sana. Zamani alichora kwenye mchanga kwa kutumia kijiti chenye ncha kali.

Alipoingia shuleni, alianza kuchora kwenye madaftari kwa kutumia penseli. Walimu wake waliipenda michoro yake na kumshika mkono katika uchoraji. Alichora nyuso za watu, alichora mazingira yenye mito, miti na milima. Alichora majumba na michoro mingi iliyowaacha watu vinywa wazi.

Shuleni, sifa zake zilizagaa sana. Hata mwalimu mkuu alimwomba achore kwenye kuta za shule, jambo alilolifanya kwa ustadi mkubwa. Mashindano ya uchoraji kuhusu utunzaji wa mazingira yalipotangazwa, mwalimu wake alipendekeza jina lake mara moja. Yeye ndiye aliyekuwa msichana pekee miongoni mwa wagombea mia moja katika gatuzi lao.

Suzana alitangazwa kama mshindi. Suzana aliwakumbusha waliomkatia tamaa kuwa kila mmoja anaweza kufanya vyema katika fani yoyote ile endapo atapewa mazingira sahihi. Vile vile, aliwakumbusha kuwa hakuna fani iliyotengewa jinsia moja tu. Alipokezwa hundi yake ya nusu milioni mbali na kupata udhamini wa masomo. Fahari ilioje!

Kifungu hiki kinazungumzia jambo gani?

  1. AMashindano ya kuchora
  2. BChangamoto za kijinsia
  3. CTalanta za wasichana
  4. DUmuhimu wa ushirikiano

Answer

B. Changamoto za kijinsia

Kifungu kinahusu Suzana akivunja dhana potovu kuwa uchoraji ni fani ya wavulana tu -- changamoto za kijinsia katika vipaji.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 6 Kiswahili questions from this test