CBC Grade 6 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 1
Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali kutoka swali la 1 hadi la 6. PAULA: Nasikitika kwamba mwaka huu pia tunashuhudia majanga yanayotokana na mvua…
From Test 16 — Karatasi ya Marudio 2026 · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Mazungumzo
Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali kutoka swali la 1 hadi la 6.
PAULA: Nasikitika kwamba mwaka huu pia tunashuhudia majanga yanayotokana na mvua nyingi za msimu wa masika. Tatizo hili ni la miaka nenda miaka rudi.
JONA: Mifugo inasombwa na maji, majengo yanaharibika na mimea mingi inang'olewa mashambani. Haya yote yatapelekea kuwepo kwa maafa mengi katika siku zijazo. Njaa, magonjwa na hata vifo viko njiani kutuandama.
PAULA: Lakini mbona hatujachukua tahadhari kama taifa kuhusu jambo hili? Kwa nini kila msimu hapa nchini tunalalamika? Ni kosa la nani hasa?
JONA: Katika msimu wa kiangazi, hali huwa ni hii hii, ukame, ukosefu wa maji, mimea kunyauka pamoja na mifugo kukosa maji na hatimaye kuangamia. Isitoshe, binadamu wengi huathirika kwa njaa na kiu. Watoto na wanawake wakiumia zaidi.
PAULA: Unadhani ni nini ambacho kinafaa kufanyika ili kuzuia hali hii mbaya?
JONA: Ni jukumu la kila mzalendo kuchukua tahadhari. Serikali huwaonya raia kuondoka katika sehemu hatari wakati wa masika lakini wao hutia nta kwenye masikio yao. Isitoshe, wakati wa kiangazi, wafugaji hushauriwa kupunguza idadi ya mifugo yao kuepuka changamoto za malisho lakini wao hupuuza tu.
PAULA: Jukumu la serikali ni lipi hasa?
JONA: Kuhakikisha kuwa inalipa suala hili kipaumbele. Kutafuta suluhisho la kudumu kwa kutenga maeneo salama ya kuwahamishia wakazi, kutafuta soko la kuuza mifugo ili kupunguza hasara inayotokana na vifo vya wanyama hawa.
JONA: Ni muhimu pia kuwahamasisha wanajamii kuhusu utunzaji wa mazingira, kuelewa mabadiliko ya tabia nchini na kuzingatia mbinu mpya za kujinufaisha kiuchumi. Tukumbuke kuwa ni vyema kutahadhari kabla ya hatari.
PAULA: Ni kweli mwenzangu, basi hata mimi na wewe tuna jukumu la kushughulikia hali hii. Kila mmoja sharti awajibike katika janga hili.
Kulingana na mazungumzo haya, ni msimu upi unaohusishwa na mvua nyingi zenye maafa?
- AKipupwe
- BMasika
- CKiangazi
- DVuli
Answer
B. Masika
Paula anasema moja kwa moja, "...majanga yanayotokana na mvua nyingi za msimu wa masika."
More Grade 6 Kiswahili questions from this test
- Paula anasema kuwa changamoto hii ya majanga imekuwa ikitokea?Question 2
- Lipi kati ya haya si tatizo ambalo linashuhudiwa katika msimu wa kiangazi kikali?Question 3
- Inapendekezwa kwamba ni nani ambaye anafaa kushughulikia hali hii?Question 4
- Kwa kutafuta soko la kuuza mifugo, serikali itakuwa ikisaidia vipi?Question 5
- Msimu wa baridi nyingi bila mvua huitwa vipi?Question 6
- Soma ufahamu unaofuata kisha ujibu swali la 7 hadi 11 Taifa la Kenya lina makabila zaidi ya arubaini na matano.…Question 7