naQonda

CBC Grade 6 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 11

Soma ufahamu ufuatao kisha ujibu maswali yanayofuata. Sungura na ng'ombe walikuwa marafiki wa kufa kuzikana kwani ushirikiano kwao ni nguvu na utengano ni…

From Test 15 — Karatasi ya Marudio 2026 · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Hadithi

Soma ufahamu ufuatao kisha ujibu maswali yanayofuata.

Sungura na ng'ombe walikuwa marafiki wa kufa kuzikana kwani ushirikiano kwao ni nguvu na utengano ni udhaifu. Marafiki hawa walikuwa na vikembe. Sungura alikuwa na vitungule wanne. Ng'ombe alikuwa na ndama mmoja wa kike.
Siku moja sungura na wanawe walikuwa wakizunguka msituni wakiwa na nia ya kupata mzabibu wale na vitungule wake wakajaribu kuyachuma mazabibu lakini hawakufua dafu. Mzabibu ulikuwa mrefu kama mlingoti. Hawangeweza kuukwea mzabibu. Mara wazo likamjia, ninaye sahibu yangu ng'ombe. Si walinena wahenga kuwa akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki?

Sungura na wanawe walienda msituni kufanya nini?

  1. AKukutana na ng'ombe
  2. BKutafuta chakula
  3. CKutembea
  4. DKuzungukazunguka

Answer

B. Kutafuta chakula

Sungura na wanawe walikwenda msituni wakiwa na nia ya kupata mzabibu na vitungule, yaani kutafuta chakula.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 6 Kiswahili questions from this test