CBC Grade 6 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 15
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata. Siku moja, wanyama wote wa msitu wa Gungumalo walikusanyika kufanya uchaguzi wa mnyama kiongozi wa…
From Test 15 — Karatasi ya Marudio 2026 · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Hadithi
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata.
Siku moja, wanyama wote wa msitu wa Gungumalo walikusanyika kufanya uchaguzi wa mnyama kiongozi wa msitu. Simba, aliyekuwa mzee na dhaifu, aliamua kustaafu. Ilikuwa ni lazima apatikane kiongozi mpya. Wanyama waliopendekezwa walikuwa:
1. Chui - alisema, ‘Mimi ni mwepesi na hodari, naweza kuwalinda wote!’
2. Tembo - akasema, ‘Nina nguvu na kumbukumbu, sitasahau shida zenu.’
3. Kobe - akasema kwa upole, ‘Mimi ni mwenye subira, naweza kusikiliza kila mmoja.’
4. Paka - alijitokeza na kusema, ‘Mimi ni safi, nitatunza msitu kama ninavyotunza manyoya yangu.’
Kura zilipopigwa, kilichowashangaza wote ni kwamba kobe ndiye alishinda! Wanyama wengi walichoka wenye haraka na kelele. Walitaka kiongozi mwenye busara, anayejali na kusikiliza. Chui alikunja mkia, tembo akatikisa masikio yake kwa mshangao na paka alifuta vumbi. Kobe alitembea pole pole hadi jukwaani na kusema kwa sauti ya utulivu, “Uongozi si kukimbia, ni kuelewa na kusuluhisha.”
Kwa nini kobe alichaguliwa kuwa kiongozi?
- AAlikuwa na marafiki wengi
- BAlikuwa na nguvu
- CAlikuwa mwenye subira na busara
- DAlikuwa mwepesi sana
Answer
C. Alikuwa mwenye subira na busara
Wanyama walitaka kiongozi mwenye busara, anayejali na kusikiliza -- sifa alizoonyesha kobe kwa upole na utulivu wake.
More Grade 6 Kiswahili questions from this test
- Kutoka swali la 16 - 20, soma kifungu kifuatacho. Kina nafasi zilizoachwa wazi. Chagua jibu lililo sahihi kati ya…Question 16
- Kutoka swali la 16 - 20, soma kifungu kifuatacho. Kina nafasi zilizoachwa wazi. Chagua jibu lililo sahihi kati ya…Question 17
- Kutoka swali la 16 - 20, soma kifungu kifuatacho. Kina nafasi zilizoachwa wazi. Chagua jibu lililo sahihi kati ya…Question 18
- Kutoka swali la 16 - 20, soma kifungu kifuatacho. Kina nafasi zilizoachwa wazi. Chagua jibu lililo sahihi kati ya…Question 19
- Kutoka swali la 16 - 20, soma kifungu kifuatacho. Kina nafasi zilizoachwa wazi. Chagua jibu lililo sahihi kati ya…Question 20
- Kamilisha sentensi hii kwa nahau sahihi. Rosa alipoingiwa na vumbi puani ___Question 21