naQonda

CBC Grade 6 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 14

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata. Siku moja, wanyama wote wa msitu wa Gungumalo walikusanyika kufanya uchaguzi wa mnyama kiongozi wa…

From Test 15 — Karatasi ya Marudio 2026 · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Hadithi

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata.

Siku moja, wanyama wote wa msitu wa Gungumalo walikusanyika kufanya uchaguzi wa mnyama kiongozi wa msitu. Simba, aliyekuwa mzee na dhaifu, aliamua kustaafu. Ilikuwa ni lazima apatikane kiongozi mpya. Wanyama waliopendekezwa walikuwa:
1. Chui - alisema, ‘Mimi ni mwepesi na hodari, naweza kuwalinda wote!’
2. Tembo - akasema, ‘Nina nguvu na kumbukumbu, sitasahau shida zenu.’
3. Kobe - akasema kwa upole, ‘Mimi ni mwenye subira, naweza kusikiliza kila mmoja.’
4. Paka - alijitokeza na kusema, ‘Mimi ni safi, nitatunza msitu kama ninavyotunza manyoya yangu.’
Kura zilipopigwa, kilichowashangaza wote ni kwamba kobe ndiye alishinda! Wanyama wengi walichoka wenye haraka na kelele. Walitaka kiongozi mwenye busara, anayejali na kusikiliza. Chui alikunja mkia, tembo akatikisa masikio yake kwa mshangao na paka alifuta vumbi. Kobe alitembea pole pole hadi jukwaani na kusema kwa sauti ya utulivu, “Uongozi si kukimbia, ni kuelewa na kusuluhisha.”

Ni nani aliyekuwa kiongozi wa zamani wa msitu?

  1. ASimba
  2. BNyani
  3. CChui
  4. DTembo

Answer

A. Simba

Kifungu kinasema simba, aliyekuwa mzee na dhaifu, aliamua kustaafu, akionyesha alikuwa kiongozi wa zamani.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 6 Kiswahili questions from this test