CBC Grade 5 Kiswahili Exam Term 1 2025 · Question 15
Kichwa kinachofaa kwa ufahamu huu ni
From Kiswahili — Monitoring Learners Progress 2025 (Set 9) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu
Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali 11-15.
Hapo zamani za kale, kinyonga hakuwa jinsi alivyo siku hizi. Alikuwa kama wanyama wengine. Hakuwa akibadilika rangi kila wakati. Siku moja, yeye na marafiki zake walialikwa katika sherehe iliyokuwa ikifanyika mjini. Yeye na wenzake waliingia katika gari na kufunga safari ya kuelekea mjini. Waliwasili mjini mwendo wa adhuhuri. Walipofika, walielekezwa mahali pa sherehe moja kwa moja. Sherehe ilipokaribia mwisho, wageni wote walielekezwa mahali pa kupata chakula. Hiyo ndiyo iliyokuwa mara ya kwanza kwa wageni waliotoka kijijini kuona matunda. Mengi walikuwa wakiyasikia tu kwenye redio na kuyaona magazetini. Kabla ya kuanza kula, walipewa onyo. Waliambiwa kuwa matunda hayo hayakuwa ya kawaida. Hakuna aliyeruhusiwa kula zaidi ya aina moja ya matunda; kuyachanganya kungeleta madhara makubwa mwilini. Kinyonga naye kutokana na tamaa, hakufuata maagizo. Alikula maembe, machungwa, maparachichi, tikitimaji bila kusahau tufaha. Ghafla, alianza kutetemeka na kuanguka chini. Aliposimama, mwili wake ulianza kubadilika rangi kulingana na rangi ya kile kilichokuwa karibu naye.
15. Kichwa kinachofaa kwa ufahamu huu ni
- ASafari ya mjini
- BMadhara ya tamaa
- CKinyonga na wenzake
- DMatunda
Answer
B. Madhara ya tamaa
Hadithi inaonyesha madhara ya tamaa ya kinyonga.
More Grade 5 Kiswahili questions from this test
- Chagua jibu sahihi la pengo 16.Question 16
- Chagua jibu sahihi la pengo 17.Question 17
- Chagua jibu sahihi la pengo 18.Question 18
- Chagua jibu sahihi la pengo 19.Question 19
- Chagua jibu sahihi la pengo 20.Question 20
- Jibu maswali yafuatayo kulingana na maagizo. Ni nomino ipi kati ya zifuatazo haipatikani katika ngeli ya LI-LI?Question 21