CBC Grade 5 Kiswahili End Term 1 Exam 2025 · Question 15
Miti ifuatayo huzaa matunda isipokuwa
From Kiswahili — End Term Assessment 2025 (Set 6) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu
Soma kifungu hiki kisha ujibu maswali 11-15.
Miti ni mapambo ya dunia. Inaponawiri na kuwa na rangi ya kijani hupendeza machoni. Huwa ni kama zulia lililofunika ardhi. Miti huvuta mvua kutoka mbali na kuzuia mmomonyoko wa udongo. Mvua ni muhimu kwa kila mmoja wetu. Mvua husaidia kukuza vyakula, hutupa maji ya kuimarisha uhai na usafi pia.
Wengi wetu hufikiri miti ni ile inayomea msituni pekee. Miti hiyo ni kama vile mwerezi, mvule, mvinje, mbambakofi na mkwaju. Mwerezi, mvule na mbambakofi hutupa mbao bora sana. Mbao hizi hutumika katika ujenzi wa kuunda vifaa kama meza, kabati, viti na vifaa vinginevyo.
Mbali na mbao na kuni, miti pia hutupa chakula. Fikiria juu ya matunda unayopenda. Matunda kama mapapai, machungwa, mapera, maparachichi na mengi mengine. Jua linapozidi ukali, watu wengi hutafuta mahali chini ya miti penye kivuli wakapumzika. Miti ikipandwa kwa mpango huwa uzio. Uzio huu unaweza kuzungushwa nyumba, shule na hata shamba. Miti huongeza urembo wa mazingira. Miti huchukua miaka mingi kuwa tayari kwa matumizi. Kwa hivyo ni wajibu wetu kuitumia miti kwa uangalifu. Tuhifadhi miti tuliyo nayo na tupande mingi zaidi.
15. Miti ifuatayo huzaa matunda isipokuwa
- AMpapai
- BMparachichi
- CMvinje
- DMpera.
Answer
C. Mvinje
Mvinje ni mti wa msituni, hauzai matunda tunayokula.
More Grade 5 Kiswahili questions from this test
- Chagua jibu sahihi la pengo 16.Question 16
- Chagua jibu sahihi la pengo 17.Question 17
- Chagua jibu sahihi la pengo 18.Question 18
- Chagua jibu sahihi la pengo 19.Question 19
- Chagua jibu sahihi la pengo 20.Question 20
- Kutoka swali la 21 hadi 30 jibu kulingana na maagizo. Ni upi si msamiati wa adabu.Question 21