CBC Grade 5 Kiswahili End Term 1 Exam 2025 · Question 14
Jina 'uzio' limepigiwa kistari. Jina hili ni sawa na
From Kiswahili — End Term Assessment 2025 (Set 6) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu
Soma kifungu hiki kisha ujibu maswali 11-15.
Miti ni mapambo ya dunia. Inaponawiri na kuwa na rangi ya kijani hupendeza machoni. Huwa ni kama zulia lililofunika ardhi. Miti huvuta mvua kutoka mbali na kuzuia mmomonyoko wa udongo. Mvua ni muhimu kwa kila mmoja wetu. Mvua husaidia kukuza vyakula, hutupa maji ya kuimarisha uhai na usafi pia.
Wengi wetu hufikiri miti ni ile inayomea msituni pekee. Miti hiyo ni kama vile mwerezi, mvule, mvinje, mbambakofi na mkwaju. Mwerezi, mvule na mbambakofi hutupa mbao bora sana. Mbao hizi hutumika katika ujenzi wa kuunda vifaa kama meza, kabati, viti na vifaa vinginevyo.
Mbali na mbao na kuni, miti pia hutupa chakula. Fikiria juu ya matunda unayopenda. Matunda kama mapapai, machungwa, mapera, maparachichi na mengi mengine. Jua linapozidi ukali, watu wengi hutafuta mahali chini ya miti penye kivuli wakapumzika. Miti ikipandwa kwa mpango huwa uzio. Uzio huu unaweza kuzungushwa nyumba, shule na hata shamba. Miti huongeza urembo wa mazingira. Miti huchukua miaka mingi kuwa tayari kwa matumizi. Kwa hivyo ni wajibu wetu kuitumia miti kwa uangalifu. Tuhifadhi miti tuliyo nayo na tupande mingi zaidi.
14. Jina 'uzio' limepigiwa kistari. Jina hili ni sawa na
- Aua
- Bmazingira
- Cmaua
- Durembo.
Answer
A. ua
Uzio ni ua unaozunguka nyumba, shule au shamba.