CBC Grade 5 Kiswahili End Term 1 Exam 2025 · Question 11
Mabasi ya shule katika nchi hii ya msimulizi yamepakwa rangi gani?
From Kiswahili — End Term 1 Assessment 2025 (Set 4) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali la 8 hadi la 14.
Mwaka huu ulipoanza, sote tulifurahi kurudi katika shule yetu. Shule hiyo inajulikana kama Mematele. Ina wanafunzi elfu moja na mia mbili na mabasi sita. Mabasi yote ya shule hiyo yamepakwa rangi ya manjano.
Tulipowasili shuleni, tuliingia madarasani na kuketi kwenye viti vyetu. Mwalimu mmoja ambaye tulimpenda sana aliingia darasani na kutuamkua, "Hamjambo wanafunzi?" Nasi tukajibu, "Hatujambo mwalimu Matunda. Shikamoo."
Kengele ilipopigwa tulielekea gwarideni. Tulisimama wima tulipokuwa tukiimba wimbo wa taifa. Baadaye mwalimu alitukagua endapo kucha zetu zilikuwa safi. Mwalimu wetu alitushauri tuwe tukinywa maji mengi kila siku ili tuwe na afya njema.
11. Mabasi ya shule katika nchi hii ya msimulizi yamepakwa rangi gani?
Answer
Manjano
"Mabasi yote ya shule hiyo yamepakwa rangi ya manjano."
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 5 Kiswahili questions from this test
- Salamu hamjambo hujibiwa hatujambo. Je, masalkheri hujibiwa aje?Question 12
- Ni nani aliwashauri wanagenzi kunywa maji mengi?Question 13
- Kwa nini wanafunzi walishauriwa kunywa maji mengi?Question 14
- Teua salamu ambayo haijaambatanishwa ipasavyo.Question 15
- Je, kati ya maneno haya katika kamusi, ni neno gani litakuwa la pili?Question 16
- Mstatili huu una maneno matano ya nomino za vitenzi-jina. Je, ni neno lipi halifai kuwa hapa?Question 17