naQonda

CBC Grade 5 Kiswahili Exam Term 1 2025 · Question 16

Taja neno lingine lenye maana sawa na barua.

From Kiswahili — School Based Assessment 2025 (Set 11B) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
(Ni asubuhi baada ya gwaride. Zubeda anabisha mlango wa ofisi ya Mwalimu Mkuu. Mwalimu anamkaribisha ndani.)
Zubeda: (Akiinama kwa heshima.) Shikamoo mwalimu?
Mwalimu mkuu: Marahaba Zubeda. Umeamkaje? Natumai kila kitu ni salama. Si kawaida yako kunitembelea ofisini asubuhi.
Zubeda: Nimeamka vyema mwalimu. Nashukuru. Hakika niliamka alfajiri. Mzazi wangu aliniamsha ili anikabidhi barua hii. (Anamkabidhi mwalimu bahasha.)
Mwalimu mkuu: Aha! Nilijua lazima una sababu ya kuja ofisini mwangu asubuhi. Barua ina ujumbe gani?
Zubeda: Sina habari. Nimepewa tu. Labda ni mwaliko au jambo. Mwalimu, ulitufunza kuwa si vyema kusoma barua za watu wengine.
Mwalimu mkuu: (Akimpongeza.) Hongera Zubeda. Wewe ni mtoto mwema. Ni vizuri kutosoma barua ambazo si zako.
Zubeda: (Akinyenyekea.) Shukran mwalimu. Mzazi wangu pia hunihimiza niwe na uaminifu kwa kuwa, heshima si utumwa.
Mwalimu mkuu: Nashukuru kwa maneno yako. Sasa unaweza kujiunga na wengine darasani. Endelea kutia bidii masomoni. Nitakupatia majibu ya barua alasiri.
Zubeda: Asante mwalimu. Kwaheri. Tutaonana wakati huo wa alasiri.
Mwalimu mkuu: Kwaheri ya kuonana.

16. Taja neno lingine lenye maana sawa na barua.

Answer

Waraka

Kisawe cha barua.

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 5 Kiswahili questions from this test