CBC Grade 5 Kiswahili Exam Term 1 2025 · Question 14
Zubeda ni mtoto mwaminifu kwa kuwa?
From Kiswahili — School Based Assessment 2025 (Set 11B) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
(Ni asubuhi baada ya gwaride. Zubeda anabisha mlango wa ofisi ya Mwalimu Mkuu. Mwalimu anamkaribisha ndani.)
Zubeda: (Akiinama kwa heshima.) Shikamoo mwalimu?
Mwalimu mkuu: Marahaba Zubeda. Umeamkaje? Natumai kila kitu ni salama. Si kawaida yako kunitembelea ofisini asubuhi.
Zubeda: Nimeamka vyema mwalimu. Nashukuru. Hakika niliamka alfajiri. Mzazi wangu aliniamsha ili anikabidhi barua hii. (Anamkabidhi mwalimu bahasha.)
Mwalimu mkuu: Aha! Nilijua lazima una sababu ya kuja ofisini mwangu asubuhi. Barua ina ujumbe gani?
Zubeda: Sina habari. Nimepewa tu. Labda ni mwaliko au jambo. Mwalimu, ulitufunza kuwa si vyema kusoma barua za watu wengine.
Mwalimu mkuu: (Akimpongeza.) Hongera Zubeda. Wewe ni mtoto mwema. Ni vizuri kutosoma barua ambazo si zako.
Zubeda: (Akinyenyekea.) Shukran mwalimu. Mzazi wangu pia hunihimiza niwe na uaminifu kwa kuwa, heshima si utumwa.
Mwalimu mkuu: Nashukuru kwa maneno yako. Sasa unaweza kujiunga na wengine darasani. Endelea kutia bidii masomoni. Nitakupatia majibu ya barua alasiri.
Zubeda: Asante mwalimu. Kwaheri. Tutaonana wakati huo wa alasiri.
Mwalimu mkuu: Kwaheri ya kuonana.
14. Zubeda ni mtoto mwaminifu kwa kuwa?
Answer
Hakusoma barua; aliifikisha kwa mwalimu mkuu
Hakufungua bahasha.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 5 Kiswahili questions from this test
- Unafikiri ni kwa nini ni makosa kusoma barua za watu wengine?Question 15
- Taja neno lingine lenye maana sawa na barua.Question 16
- Mti huu una nomino zifuatazo: furaha, uzi, hekima, ukarimu, werevu. Chagua nomino ambayo si ya dhahania kwenye mti huu:Question 17
- Andika sentensi ifuatayo katika hali ya wingi. Unyoya wa kuku yule ni mweupe.Question 18
- Chagua sentensi yenye nomino iliyo katika ngeli ya I-ZIQuestion 19
- Tazama picha hii. Huyu ni Rhoda. Rhoda anasoma kitabu cha hadithi. Tunga sentensi ukianza kwa: Kusoma kwake ___.Question 20