naQonda

CBC Grade 5 Kiswahili End Term 1 Exam 2025 · Question 12

Soma kifungu hiki kwa sauti.

From Kiswahili — End Term 1 Exam 2025 (Set 3) — Kusikiliza, Kuzungumza na Kusoma · 10 marks · Topic: Kusoma, Kusoma kwa Sauti

Kasuku wangu anaitwa Pendo. Nilipewa Pendo kama zawadi na mwalimu wangu baada ya kuupita mtihani. Mwalimu wangu alinifunza jinsi ya kumtunza Pendo ili awe mwenye afya na furaha. Koko yangu alimjengea Pendo tundu lenye nafasi ya kutosha ili Pendo aweze kucheza akiwa humo ndani. Mara kwa mara mimi humtoa Pendo tunduni na kucheza naye.
Pendo hupenda sana kula majani mabichi, viazi vitamu, karoti na matunda. Pendo hufurahi sana kila ninapomwosha. Yeye hurukaruka kwa furaha huku akicheza na maji. Baada ya kumwosha Pendo mimi huvisafisha vyombo anavyotumia kuoga kwa maji safi kisha kuvianika juani.
Daktari wa mifugo huja kumchunguza na kumtibu Pendo kila anapougua. Nampenda sana Pendo wangu.

Soma kifungu hiki kwa sauti.

Answer

Kasuku wangu anaitwa Pendo. Nilipewa Pendo kama zawadi na mwalimu wangu baada ya kuupita mtihani. Mwalimu wangu alinifunza jinsi ya kumtunza Pendo ili awe mwenye afya na furaha. Koko yangu alimjengea Pendo tundu lenye nafasi ya kutosha ili Pendo aweze kucheza akiwa humo ndani. Mara kwa mara mimi humtoa Pendo tunduni na kucheza naye. Pendo hupenda sana kula majani mabichi, viazi vitamu, karoti na matunda. Pendo hufurahi sana kila ninapomwosha. Yeye hurukaruka kwa furaha huku akicheza na maji. Baada ya kumwosha Pendo mimi huvisafisha vyombo anavyotumia kuoga kwa maji safi kisha kuvianika…

Soma kwa ufasaha na kwa sauti inayosikika; tamka vizuri maneno kama kumtunza, alimjengea, tunduni, hurukaruka, huvisafisha na kumchunguza.

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 5 Kiswahili questions from this test