CBC Grade 5 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 4
Amani alimsaidiaje Zawadi kuelewa?
From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 7) · 1 mark · Topic: Kusoma, Mazungumzo
Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu swali la 1 hadi 5.
Amani: Habari Zawadi? Leo somo la Kiswahili lilikuwa zuri sana, sivyo?
Zawadi: Ni kweli? Amani. Lakini kuna sehemu imenichanganya kidogo.
Amani: Ipi hiyo?
Zawadi: Hii ya nomino dhahania. Sijaelewa kabisa.
Amani: Usijali, ninakusaidia. Kwanza, unakumbuka aina nyingine za nomino tulizofunzwa?
Zawadi: Ndio, kuna nomino za pekee kama Juma na Nairobi, na nomino za kawaida kama mtoto na meza.
Amani: Vizuri sana! Sasa, nomino dhahania ni majina ya vitu ambavyo huwezi kuviona au kuvishika.
Zawadi: Unamaanisha kama nini?
Amani: Mfano ni upendo, furaha, au hasira. Hivi vitu vipo lakini huwezi kuvishika kwa mkono.
Zawadi: Aah! Sasa naanza kuelewa kwa hivyo, furaha ni nomino dhahania kwa sababu ni hisia?
Amani: Ndio!
Zawadi: Asante sana Amani, sasa nimeelewa.
Amani: Karibu sana! Ukielewa nomino hizi, Kiswahili kitakuwa rahisi zaidi.
4. Amani alimsaidiaje Zawadi kuelewa?
- AKwa kumpa vitabu.
- BKwa kumpa mifano.
- CKwa kumwambia aulize mwalimu.
- DKwa kumwambia aache somo.
Answer
B. Kwa kumpa mifano.
Alitoa mifano.