naQonda

CBC Grade 5 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 3

Ni ipi kati ya hizi ni nomino dhahania?

From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 7) · 1 mark · Topic: Sarufi na Matumizi ya Lugha, Nomino

Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu swali la 1 hadi 5.
Amani: Habari Zawadi? Leo somo la Kiswahili lilikuwa zuri sana, sivyo?
Zawadi: Ni kweli? Amani. Lakini kuna sehemu imenichanganya kidogo.
Amani: Ipi hiyo?
Zawadi: Hii ya nomino dhahania. Sijaelewa kabisa.
Amani: Usijali, ninakusaidia. Kwanza, unakumbuka aina nyingine za nomino tulizofunzwa?
Zawadi: Ndio, kuna nomino za pekee kama Juma na Nairobi, na nomino za kawaida kama mtoto na meza.
Amani: Vizuri sana! Sasa, nomino dhahania ni majina ya vitu ambavyo huwezi kuviona au kuvishika.
Zawadi: Unamaanisha kama nini?
Amani: Mfano ni upendo, furaha, au hasira. Hivi vitu vipo lakini huwezi kuvishika kwa mkono.
Zawadi: Aah! Sasa naanza kuelewa kwa hivyo, furaha ni nomino dhahania kwa sababu ni hisia?
Amani: Ndio!
Zawadi: Asante sana Amani, sasa nimeelewa.
Amani: Karibu sana! Ukielewa nomino hizi, Kiswahili kitakuwa rahisi zaidi.

3. Ni ipi kati ya hizi ni nomino dhahania?

  1. AMeza
  2. BKitabu
  3. CFuraha
  4. DKalamu

Answer

C. Furaha

Furaha ni hisia.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 5 Kiswahili questions from this test