CBC Grade 5 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 13
Chagua mapambo ya kisasa peke yake.
From Kiswahili — Revision 2026 (Booklet 6) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu
Soma hadi ufahamu ufuatao kisha ujibu maswali yafuatayo.
Vifaa au vitu mbalimbali vinavyofanya miili yetu ionekane nadhifu na ya kuvutia huitwa mapambo. Tangu zamani, jamii mbalimbali zimetumia mapambo asili kama vile shanga, herini na vikuku. Mapambo haya huundwa kutoka kwa ngozi, miti au udongo. Mapambo si ya urembo tu, bali huwakilisha utamaduni na imani za watu hasa wakati wa sherehe za kitamaduni na harusi.
Katika maisha ya kisasa, kuna aina nyingi ya mapambo kama vile vipuli, mkufu, pete, saa na kipini ambazo hupendwa na watu wa rika zote. Ni muhimu kuchagua mapambo yanayoambatana na mavazi yetu ili kuleta mpangilio mzuri wa rangi na mtindo. Ukumbuke kuwa pambo kuu la kudumu ni usafi wa mwili na tabia njema. Urembo wa nje hupendeza zaidi ikiwa mtu ni mnyenyekevu na mwenye adabu.
13. Chagua mapambo ya kisasa peke yake.
- AVipuli na mkufu
- BHerini na saa
- CKipini na vikuku
- DShanga na pete
Answer
A. Vipuli na mkufu
Vipuli na mkufu ni ya kisasa.
More Grade 5 Kiswahili questions from this test
- Ni nini maana ya msemo “kukata tamaa”?Question 14
- Kwa jumla, ufahamu huu unazungumzia nini?Question 15
- Chagua nomino ya kipekee katika maneno yafuatayoQuestion 21
- Jina ‘makiwa’ hutumiwa vipi?Question 22
- Andika sentensi hii katika umoja Nyumba hizi zinajengwaQuestion 23
- Kamilisha nomino hii ya makundi. baraza la ___Question 24