CBC Grade 4 Kiswahili Mid Term 1 Exam 2025 · Question 12
Nyumba yetu ina vyumba vingapi?
From Kiswahili — KPSEA Midterm Assessment 2025 Set 2 (Lugha) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Kifungu
Soma kifungu hiki kisha ujibu swali la 11 - 15.
Nyumba yetu si kubwa sana. Kuta zake ni za mawe. Ina madirisha mengi na milango mitano. Ina paa la bati. Madirisha ni ya mbao na vyuma. Madirishani kuna mapazia ya rangi nyeupe na sakafuni kuna zulia la samawati. Nyumba yetu ina vyumba vingi sana.
Kuna sebule ambayo iko karibu na chumba cha kulala au malazi. Chumba cha kupikia ni jikoni, cha kuogea ni bafu na pia kuna msala. Ndani ya nyumba yetu mna runinga, viti, vitanda, makochi, redio, simu, kabati, meza na vyombo vingine vya jikoni.
12. Nyumba yetu ina vyumba vingapi?
- AVitano
- BVitatu
- CSita
- DViwili.
Answer
A. Vitano
Kifungu kinataja sebule, chumba cha kulala, jiko, bafu na msala. Hivyo ni vyumba vitano.