CBC Grade 4 Kiswahili Mid Term 2 Exam 2025 · Question 2
Tumeambiwa kuwa chakula chetu lazima kiwe na
From Kiswahili — Term 2 Midterm Assessment 2025 (Set 10) (Lugha) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Kifungu
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 1 hadi 3.
Kuna umuhimu mkuu wa kudumisha afya bora. Binadamu akiwa na afya bora, huweza kufanya shughuli zote vizuri na kwa wakati unaofaa. Ili kuwa na afya bora, ni vizuri kuzingatia lishe bora. Chakula tunachokila lazima kiwe na kabohaidreti, protini na vitamini kwa viwango vinavyofaa mwilini. Vile vile, ni vizuri kunywa maji safi na salama kila siku. Je, wajua kuwa matunda hutukinga tusiwe wagonjwa? Wapishi na watu wote wanaoandaa chakula ni lazima wawe safi ili tusipatwe na magonjwa.
2. Tumeambiwa kuwa chakula chetu lazima kiwe na
- Asukari na chumvi nyingi.
- Bkabohaidreti, protini na vitamini.
- Cmafuta mengi pekee.
- Dmatunda pekee.
Answer
B. kabohaidreti, protini na vitamini.
"Chakula tunachokila lazima kiwe na kabohaidreti, protini na vitamini kwa viwango vinavyofaa mwilini."