CBC Grade 4 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 6
Ni nini maana ya nahau amekula chumvi nyingi?
From Kiswahili — Revision Paper 1 (2026) (Lugha) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Kifungu
Soma kifungu hiki kisha ujibu swali la 6 hadi la 9.
Mzee Busara alikuwa amekula chumvi nyingi. Yaani alikuwa amezeeka sana. Moja ya sifa zake kuu kijijini ilikuwa ni kusimulia hadithi. Matamshi yake yalikuwa bora, nayo sauti yake ilikuwa kama ya ninga. Wakati wa jioni wajukuu wake walimzingira ili kupata uhondo wa hadithi zake zisizo na mwisho. Mara nyingi hadithi zake zilihusu jinsi ambavyo watu wa kitambo waliishi. Wajukuu wake walizidi kufurahia kila siku kwa sababu hadithi za babu yao ziliwachangamsha na kuwarekebisha kitabia.
Ni nini maana ya nahau amekula chumvi nyingi?
Answer
Kuzeeka au kuwa na miaka mingi.
Kifungu kinaeleza nahau hii mara moja: "Yaani alikuwa amezeeka sana." Kula chumvi nyingi ni kuishi miaka mingi.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.