naQonda

CBC Grade 4 Kiswahili Revision Exam 2026 · Question 5

Mwuzaji alifaa kumpa Teya pesa ngapi?

From Kiswahili — Revision Paper 1 (2026) (Lugha) · 1 mark · Topic: Kusikiliza na Kuzungumza, Ufahamu wa Mazungumzo

Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu swali la 1 hadi la 5.

(Ni sokoni, Teya anapita sokoni akitoka kazini)

Teya: Umeshindaje? Naona unazo mboga zinazovutia kwelikweli. Bei gani fungu hili?
Mwuzaji: Vyema sana mwenzangu. Hizi nimezivuna kutoka shambani mwangu leo. Pia kuna nyanya, pilipili, vitunguu na karoti. Leo, siku zote bei hutegemea mapatano.
Teya: Hahaha! Leo wateja wote watapitia hapa kibandani pako. Haya naomba uniuzie mafungu mawili ya sukumawiki na....
Mwuzaji: Samahani dada. Natumai unajua bei ya mwaka huu mpya. Fungu moja la sukumawiki sasa ni shilingi ishirini.
Teya: Gharama ya maisha nayo! Niuzie mafungu mawili ya sukumawiki, fungu moja la nyanya na vitunguu fungu moja.
Mwuzaji: Karoti leo?
Teya: Bado zipo. Nilinunua nyingi. Vyote ni shilingi ngapi?
Mwuzaji: Naam, vyote ni shilingi themanini.
Teya: Shika noti ya mia moja unipe salio.

Mwuzaji alifaa kumpa Teya pesa ngapi?

  1. AShilingi themanini
  2. BShilingi ishirini
  3. CShilingi mia moja
  4. DShilingi hamsini

Answer

B. Shilingi ishirini

Teya alitoa noti ya shilingi mia moja kwa bidhaa za shilingi themanini. Salio ni 100 − 80 = shilingi ishirini.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 4 Kiswahili questions from this test