naQonda

CBC Grade 9 Kiswahili Opener Exam Term 1 2025 · Question 40

Mwandishi wa dondoo hii ametumia mbinu mbalimbali za lugha. Huku ukitolea mifano mwafaka, taja mbinu zozote tatu kati ya hizo.

From Test 121 — Kiswahili Mukula wa 1 2025 · 3 marks · Topic: Fasihi, Tamthilia

Soma/Read the source text, then answer.
(Bi Fauzia na mumewe, Bwana Hemedi, wameketi sebuleni wakizungumza.)

Bi Fauzia: (akimpa dawa na glasi ya maji) Maji ndiyo haya mume wangu. Daktari alisema umeze dawa kwa wakati unaofaa. Utapata nafuu baada ya muda.
Bwana Hemedi: Vipi kuhusu Yakobo? Alisema atakuja kuniona lini? Au anangoja kuja kulia kwenye matanga yangu?
Bi Fauzia: Huyo mtoto wetu wa kiume simwelewi tena. Kila siku anasema amebanwa na kazi. Kazi gani hii inayomsukuma mtoto kuwatelekeza wazee wake?
Bwana Hemedi: Si neno. Angaa tunaye Suluhu. Nani angesema mtoto wa kike angekuja kutufaa? Licha ya dhuluma nyingi tulizomfanyia siku zile bado ana moyo wa kutuhurumia. Mola atambariki leo na kesho ahera… (anadondokwa na machozi)
Bi Fauzia: Hayo yameshapita, yaliyopita si ndwele mume wangu. Mwenyewe Suluhu alishakusamehe kitambo. Huoni yuko radhi kugharamia hata matibabu yako!
Bwana Hemedi: Siku zile niling’ang’ania kumwoza kwa Mzee Kizito. Tamaa ilikuwa imenifumba macho nusura nimtumbukize mwanangu kisimani. Nilikuwa kipofu kama jongoo. Hivi leo binti yangu angekuwa wapi?
Bi Fauzia: Nakumbuka mzee huyo alituacha mkono baadaye kutokana na maradhi ya ukimwi. Maskini mabinti waliovutiwa na mali yake. Wengi wao ni ng’onda siku hizi. Wengine wameshamfuata katika safari isiyo na marejeo.
Bwana Hemedi: Bora utawala wetu ulishikilia kikiki wito wa kutaka mabinti wote waelimishwe. Hao kaka zao tuliowategemea wanatufaa vipi siku hizi?
Bi Fauzia: Uongozi thabiti ni msingi wa maendeleo. Lau viongozi wetu wasingekuwa waona mbele, jamii yetu ingekuwa bado imezama katika giza la mila potovu. Au wasemaje?
Bwana Hemedi: Hayo ni kweli mke wangu. Haya naomba nipumzike kidogo. Dawa hii inanitia kizunguzungu.
Bi Fauzia: Pumzika mume wangu (anatazama jikoni). Hebu nami nikakuandalie chajio. Sitaki dawa hiyo ikuzidie nguvu.

Mwandishi wa dondoo hii ametumia mbinu mbalimbali za lugha. Huku ukitolea mifano mwafaka, taja mbinu zozote tatu kati ya hizo.

Answer

Methali—‘yaliyopita si ndwele’; tashbihi—‘kipofu kama jongoo’; nahau/sitiari—‘tamaa ilikuwa imenifumba macho’ au ‘nimtumbukize mwanangu kisimani’; maswali ya balagha—‘Hao kaka zao tuliowategemea wanatufaa vipi?’ Hoja zozote tatu zenye mifano zikubalike.

A complete answer could be: Methali—‘yaliyopita si ndwele’; tashbihi—‘kipofu kama jongoo’; nahau/sitiari—‘tamaa ilikuwa imenifumba macho’ au ‘nimtumbukize mwanangu kisimani’; maswali ya balagha—‘Hao kaka zao tuliowategemea wanatufaa vipi?’ Hoja zozote tatu zenye mifano zikubalike.

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 9 Kiswahili questions from this test