CBC Grade 9 Kiswahili Opener Exam Term 1 2025 · Question 2
Unafikiria ni kwa nini Maria hakutaka mama yake aje shuleni?
From Test 121 — Kiswahili Mukula wa 1 2025 · 1 mark · Topic: Kusoma, Kusoma kwa Ufahamu
Soma/Read the source text, then answer.
Maria alikuwa msichana mwerevu. Alisomea katika shule ya Elimubora. Walimu na wanafunzi walimpenda kutokana na werevu na ukarimu wake. Kila siku marafiki hao walimganda kama kupe.
Jambo la ajabu ni kuwa hakuna mtu aliyewajua wazazi wa Maria. Kila mara kulipokuwa na mkutano wa wazazi, Maria alitoa visingizio vya kila aina. Mara alisema kuwa mama yake alikuwa mgonjwa au ameenda safarini. Hakutaka rafiki yeyote amtembelee kwao.
Siku moja rafiki yake anayeitwa Shamila alimfuata kisirisiri hadi kwao. Mama yake alisikia mlango ukibishwa akafungua. Hapo ndipo Shamila alipoelewa ni kwa nini Maria hakutaka mama yake aonekane. Alikuwa na alama nyingi usoni zilizoachwa na majeraha ya moto.
Mama aliandaa chai akawamiminia Shamila na Maria. Alianza kuwasimulia kisa cha miaka kadhaa iliyopita. Aliwaeleza kuhusu mama mmoja ambaye aliingia katika nyumba iliyokuwa ikichomeka ili amwokoe binti yake. Alifaulu kumtolea mtoto huyo dirishani lakini yeye hakuwa na bahati. Alichomeka vibaya alipokuwa akitoka kwani hakuwa na budi kupitia kwenye moto.
“Mtoto huyo ana bahati sana. Mama yake alijitoa mhanga ili amwokoe. Ama kweli uchungu wa mwana aujuaye ni mama,” Shamila alisema kwa masikitiko.
Mama Maria aliingia chumbani akatoka na picha ya msichana mrembo kama hurulaini. “Je, mnatambua aliye pichani?” aliwauliza mabinti wale. Maria alitazama picha ile kwa makini. Mara moja alitambua kidani ambacho mama yake alipenda kuvaa. Ghafla akajua yaliyojiri. Kumbe mama yake alipoteza uzuri wake akimwokoa.
“Nisamehe mama,” alilia huku akimkumbatia mamaye. Tangu siku hiyo, alimwona mama yake kama shujaa wake. Aliandamana naye kila mahali. Aligundua kuwa urembo wa kweli haumo kwenye sura bali matendo yetu.

Answer
Aliogopa au aliaibika marafiki wangeona makovu ya moto usoni mwa mama yake.
A complete answer could be: Aliogopa au aliaibika marafiki wangeona makovu ya moto usoni mwa mama yake.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 9 Kiswahili questions from this test
- Picha aliyoleta Mama Maria ilikuwa ya nani?Question 3
- Umejifunza nini kutokana na hadithi hii?Question 4
- Kulingana na kifungu, polisi wakifumbia macho visa vya utovu wa usalamaQuestion 5
- Jukumu la kudumisha usalama ni la nani kulingana na kifungu?Question 6
- Methali ‘kinga ni bora kuliko tiba’ imetumika kwa maana gani katika kifungu?Question 7
- Neno ‘hongo’ limetumika katika kifungu. Kisawe cha neno hili niQuestion 8