CBC Grade 6 Kiswahili Opener Exam Term 3 2026 · Question 3
Mkulima mzuri huwekeza kwa kununua nini ili kurahisisha kazi yake?
From Test 3 — Term 3: First Assessment 2026 (Kiswahili Lugha) · 1 mark · Topic: Kusikiliza na Kuzungumza, Ufahamu wa Mazungumzo
Mazungumzo kati ya Chacha na Mawia
(Chacha anazungumza na rafiki yake Mawia.)
Chacha: Je, ungependa kufanya kazi gani baada ya kukamilisha masomo yako?
Mawia: Ningependa sana kuwa rubani. Marubani hulipwa mshahara mzuri sana na hawachoki kwa kufanya kazi ngumu. Je, wewe ungependelea kuwa nani?
Chacha: Ninatamani sana kuwa mkulima. Nalipenda sana somo la zaraa.
Mawia: (Akishangaa) Ala! Ukulima ni kazi kweli? Unataka kuishi ukiwa mchafu? Ukulima sio kazi nzuri hata kidogo.
Chacha: Kwa nini unasema si kazi nzuri?
Mawia: Kazi hiyo inachosha sana. Aidha, wakulima wengi ni maskini hohehahe.
Chacha: Hapo sikubaliani nawe kabisa, ndugu yangu. Ukulima ni kazi kama nyingine yoyote. Wapo wakulima wenye mali nyingi hata kuliko viongozi wakuu serikalini.
Mawia: (Akiwa na shauku) Enhee! Hebu nieleze zaidi, rafiki yangu.
Chacha: Mkulima mzuri huwekeza kwa kununua pembejeo za kilimo. Anaweza kununua mitambo ya kulima, kupalilia, kuvuna na hata kunyunyizia dawa. Sio lazima asagike kwenye mpini wa jembe kila siku.
Chacha: Si hayo tu, ukitumia mbinu za kisasa za kilimo, unaweza kujiongezea kipato kikubwa bila hata kuwa na shamba kubwa. Teknolojia mpya imechangia kuvumbuliwa kwa mbegu zinazostahimili ukame na vimelea. Kwa hivyo, mkulima huhakikishiwa mazao bora wakati wote.
Mawia: Kumbe! Nimekuwa na mtazamo tofauti sana kuhusu kilimo. Sasa umenifumbua macho. Sasa nakuunga mkono kikamilifu. Nimegundua kuwa una maarifa ya kutosha kuhusu kilimo.

- APembejeo za kilimo
- BShamba kubwa
- CMavazi mazuri
- DMbegu nyingi
Answer
A. Pembejeo za kilimo
Jibu sahihi ni A. Chacha anasema, "Mkulima mzuri huwekeza kwa kununua pembejeo za kilimo." Kisha anataja mitambo ya kulima, kupalilia, kuvuna na kunyunyizia dawa kama mifano ili kazi iwe rahisi. Shamba kubwa, mavazi mazuri na mbegu nyingi hazitajwi kama kitu anachowekeza mkulima mzuri.
More Grade 6 Kiswahili questions from this test
- Mbegu zilizovumbuliwa kwa teknolojia mpya zinasaidia kukabiliana na nini?Question 4
- Neno "zaraa" jinsi lilivyotumika katika mazungumzo lina maana sawa na:Question 5
- Chagua jibu lililo sahihi kulingana na aya ya kwanza:Question 6
- Ipi si sifa ya panya kulingana na kifungu hiki?Question 7
- Ni jambo lipi linaloonyesha ukatili au dhuluma kwa wanyama kulingana na kifungu hiki?Question 8
- Kichwa kifaacho zaidi kwa kifungu hiki ni:Question 9