CBC Grade 2 Kiswahili Mid Term 3 Exam 2025
Kiswahili — Mid-Term Assessment 2025 (Set 13) · Mid-Term Assessment 2025 (Set 13) · 33 questions
Topics: Kusikiliza na Kuzungumza, Kusoma, Sarufi na Matumizi ya Lugha, Kuandika.
All 33 questions with answers
- Question 1: ZOEZI A Jibu maswali kwa sauti. 1. Mahali ambapo watu hupata matibabu ni wapi?Answer: Hospitalini.
- Question 2: Ni vitu gani hupatikana hospitalini?Answer: Dawa na vitanda.
- Question 3: Maziwa yana rangi ipi?Answer: Nyeupe.
- Question 4: Watu huvalia nini wakati wa jua?Answer: Kofia na nguo nyepesi.
- Question 5: Taja haki mbili za watoto.Answer: Elimu na chakula.
- Question 6: ZOEZI B: KUSOMA KWA SAUTI 1. Soma kifungu kifuatacho kwa sauti.Answer: Familia ya Bwana Juma ina watoto watatu. Watoto hawa ni Amani, Neema na Baraka. Bwana Juma ni daktari. Mama…
- Question 7: Soma sentensi hizi kwa sauti.Answer: Ninapenda kula matunda matamu. Baba yangu huenda kazini kila siku. Wanafunzi wanapenda kucheza michezo.…
- Question 8: (a) Sebuleni kulikuwa na vitu gani?Answer: viti vya starehe na meza nzuri
- Question 9: (b) Familia ilikusanyika kufanya nini?Answer: kucheka na kuzungumza kuhusu siku ilivyokuwa
- Question 10: (c) Ukutani kulikuwa na nini?Answer: picha za familia
- Question 11: (d) Je, watoto waliketi wapi?Answer: kwenye mkeka
- Question 12: (e) Keki ilipoletwa watu walifanya nini?Answer: walifurahi
- Question 13: Kanusha sentensi hizi. a) Wewe ulisoma.Answer: Wewe hukusoma.
- Question 14: b) Wewe ulicheza.Answer: Wewe hukucheza.
- Question 15: c) Wewe ulilala.Answer: Wewe hukulala.
- Question 16: d) Wewe uliimba.Answer: Wewe hukuimba.
- Question 17: e) Wewe ulisafiri.Answer: Wewe hukusafiri.
- Question 18: Tumia 'huu' au 'hii' kujaza pengo. a) Mti ___ unapendeza.Answer: A. huu
- Question 19: b) Nyumba ___ ni yetu.Answer: B. hii
- Question 20: c) Uwanja ___ una watu wengi.Answer: A. huu
- Question 21: d) Kalamu ___ ni yangu.Answer: B. hii
- Question 22: e) Mkono ___ umevunjika.Answer: A. huu
- Question 23: Tumia 'vizuri', 'vibaya', 'polepole' au 'haraka'. a) Dada alitembea barabarani ___ akapata ajali.Answer: D. haraka
- Question 24: b) Kobe ni mnyama anayetembea ___Answer: C. polepole
- Question 25: c) Ukitembea ___ unaweza kuumia mguu.Answer: B. vibaya
- Question 26: d) Mtoto alilala kitandani ___ hakuanguka.Answer: A. vizuri
- Question 27: e) Mama alipika chakula hiki ___ tukakula chote.Answer: A. vizuri
- Question 28: Andika kinyume. a) ChekaAnswer: lia
- Question 29: b) LalaAnswer: amka
- Question 30: c) KetiAnswer: simama
- Question 31: d) PandaAnswer: shuka
- Question 32: e) VaaAnswer: vua
- Question 33: SEHEMU YA 4: KUANDIKA Andika sentensi tano kuhusu 'RAFIKI YANGU'.Answer: Rafiki yangu anaitwa Neema. Ana miaka saba. Tunasoma darasa moja. Tunacheza pamoja. Ninampenda rafiki yangu.