naQonda

CBC Grade 9 KJSEA Kiswahili Practice Exam · Question 1

Kulingana na kifungu ni kweli kuwa:

From Test 84 — Kiswahili Paper 1 (KJSEA) · 1 mark · Topic: Kusoma, Kusoma kwa Ufahamu

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali kuanzia la 1 hadi la 6.
Kilimo ni miongoni mwa sekta muhimu humu nchini. Tangu jadi wakulima wamekuwa wakitegemea mvua katika shughuli zao za kilimo. Udongo wenye rotuba na hali nzuri ya anga imekuwa ikifanikisha shughuli za kilimo. Wakulima wamekuwa wakivuna mazao mengi na hatta wafugaji wamefaidi kutokana na kilimo. Ni dhahiri kuwa hali ya anga huletea wakulima faida na hasara. Ipo misimu inayowaliza wakulima na mingine huwasononesha.

Licha ya changamoto zinazowakabili wakulima, wakulima wamepata afueni siku za hivi karibuni. Teknolojia mpya imechangia pakubwa kuimarisha sekta hii. Mbegu huteuliwa ifaavyo, mbolea na aina ya ardhi inayofaa katika upanzi wa mimea husika. Hali ya kupanda na kungoja kwa hamu na ghamu mbingu zifunguke ishapitwa na wakati. Mimea hunyunyiziwa maji msimu wa kiangazi. Ni muhali kupanda mimea kwenye udongo usiofaa iwapo unakumbatia kilimo cha kisasa.

Hata hivyo, inasikitisha kuona jinsi ambavyo baadhi ya vijana wanavyopuuza sekta hii muhimu. Yamekuwa mazoea kwa baadhi ya vijana kuwakejeli wenzao wanaojihusisha na kilimo. Isitoshe, wengine huwakejeli mitandaoni bila soni. Ajabu ni kwamba wanaofanya hivyo ni wakubwa kwa wadogo, wake kwa waume.

Jambo linalotia moyo ni namna ambavyo shule zetu na vyuo vinavyochangia ukuaji wa sekta hii. Utafiti vyuoni na mafunzo ya mbinu za kisasa ni vichocheo vya maendeleo katika sekta ya kilimo. Serikali nayo imejifunga kibwebwe kuhakikisha kuwa barabara zilizoharibika zimekarabatiwa na miundo mbinu yote kuimarishwa. Bidhaa husafirishwa kutoka mashambani hadi masokoni bila matatizo.

Vyama vya ushirika vimebuniwa na vimehakikisha kuwa wakulima wanapokea pembejeo kwa wakati ufaao. Wizara ya kilimo nayo haijaachwa nyuma. Imekuwa katika mstari wa mbele kuhakikisha kuwa wakulima wanapata mbolea kwa bei nafuu. Visingizio na vizingiti vya kutojiinua kihali katika sekta ya kilimo sasa vimeondolewa. Tusididimize kilimo maadamu ndicho uti wa mgongo wa taifa letu.

1. Kulingana na kifungu ni kweli kuwa:

  1. AA. Idadi kubwa ya wananchi wanategemea kilimo
  2. BB. Zamani wakulima walinyunyizia mashamba maji
  3. CC. Ni wakulima tu wanaofaidika na kilimo
  4. DD. Vijana hawapendi shughuli zinazohusiana na kilimo

Answer

A. A. Idadi kubwa ya wananchi wanategemea kilimo

Jibu sahihi: A. Idadi kubwa ya wananchi wanategemea kilimo.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 9 Kiswahili questions from this test