CBC Grade 8 Kiswahili Opener Exam Term 3 2026 · Question 4
Kwa jumla, watakaochangia uadilifu shuleni ni wafuatao isipokuwa
From Kiswahili — Term 3 Opener Assessment 2026 (Set 11) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Makala
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali la 1 hadi la 6.
Uadilifu ni jambo la busara na kupendeza kwa mwanadamu yeyote yule. Taifa likiwa na wananchi wenye maadili, bila shaka laweza kupiga hatua mbele kwa kasi kuliko lenye raia wasioadilifu. Udongo wenye rutuba huzaa mazao yaliyonawiri, usio na rutuba mazao huvia na kunyauka.
Uadilifu huleta uwajibikaji, uwekevu, ustahimilivu, unyofu, uongofu na hulka nyingine za kuvutia. Je, mbona wanafunzi katika baadhi ya shule wanaonyesha tabia zisizofaa kama vile uchomaji wa shule, kutowaheshimu walimu na matumizi ya dawa za kulevya? Ni ukosefu wa vielelezo vyema au ni kizazi kisichoshinda mwadhifu wala mtekamaji msikitini? Waelekezi wameshindwa na kazi zao au wanafunzi hawa wamevimba vichwa kiasi cha kutoambilika?
Penye moshi sharti pawe na moto. Ukosefu huu wa nidhamu unaashiria utepetevu wenye kina kirefu katika jamii. Wanafunzi hawa huthibitisha ukosefu wa ustaarabu kwa migomo ya kila wakati, uharibifu mkubwa wa mali shuleni. Huu ni ukatili usioweza kukubalika katika jamii ya sasa.
Mwanzo kabisa ni vyema kuwepo na kutumia njia za mawasiliano kati ya wanafunzi na viongozi wa shule. Walimu wakuu, walimu, viranja na wanafunzi kwa jumla wasemezane ili hali inapozuka, suluhu ipatikane kabla ya maji kuzidi unga. Aidha shule ziwe zimeshirikisha washauri nasaha katika shughuli za kuwaelekeza wanafunzi.
Jamii pia ina jukumu la kuwaelekeza wana wao kwa njia ya mfano mwema wa kuigwa. Ulevi na utumiaji wa mihadarati uliokithiri katika baadhi ya jamii ukashifiwa vikali. Viongozi wa dini nao wakaze kamba kuhubiri na kuwafunza waumini maadili.
4. Kwa jumla, watakaochangia uadilifu shuleni ni wafuatao isipokuwa
- Awalimu
- Bwanafunzi
- Cviranja
- Dviongozi wa kitaifa
Answer
D. viongozi wa kitaifa
Kifungu kinataja walimu wakuu, walimu, viranja, wanafunzi, washauri nasaha, jamii na viongozi wa dini; viongozi wa kitaifa hawatajwi.
More Grade 8 Kiswahili questions from this test
- Jukumu la viongozi wa dini kulingana na kifungu niQuestion 5
- Ukosefu wa nidhamu shuleni unaonyeshwa kupitiaQuestion 6
- Mwandishi anaanza kwa kusema kuwa mazingira ni mamboQuestion 7
- Kati ya haya, ni lipi lisiloathiriwa na mazingira?Question 8
- Kulingana na maoni ya mwandishi kuhusu mtoto,Question 9
- Mtoto anayekua akishuhudia watu wakipigana na kuumizana,Question 10