naQonda

CBC Grade 8 Kiswahili Opener Exam Term 3 2026 · Question 10

Mtoto anayekua akishuhudia watu wakipigana na kuumizana,

From Kiswahili — Term 3 Opener Assessment 2026 (Set 11) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Makala

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali la 7 hadi la 12.

Mazingira ni jumla ya mambo yanayomzunguka binadamu. Ni mambo ambayo hutokea kuwa sehemu ya maisha ya mja kuanzia kwenye tabia, mienendo, imani, itikadi na hata afya. Wengi husema kuwa mazingira ni kiungo cha maisha.

Mtoto anapozaliwa katika mazingira yaliyojaa uhuni na uhalifu, huenda kikawa vigumu kumwelekeza mtoto kama huyu katika kutenda mema. Kumbuka amezoea kuwaona watu wakipigana, wakiumizana na kutoana damu. Je, ana imani gani kuhusu amani na utangamano?

Mazingira aidha yanaweza kuathiri utendaji kazi wa mtu. Mtu aliyelelewa katika mazingira ya ulevi hatafanya juhudi kubwa kuishi bila ya kuwa mraibu kwani dunia yake wakati wa ukuaji wake ilisheheni ulevi. Mtoto wa aina hii hujua kila aina ya matusi kwa kuwa mazingira yake yalijaa wenye vinywa vichafu kila wakati.

10. Mtoto anayekua akishuhudia watu wakipigana na kuumizana,

  1. Ahawezi kuelewa umuhimu wa ghasia.
  2. Bhukosa kuona thamani ya amani na utangamano.
  3. Chuwa na kinywa kichafu.
  4. Dhuwa na wepesi wa kukataa pombe.

Answer

B. hukosa kuona thamani ya amani na utangamano.

Mwandishi anauliza mtoto aliyezoea kuona watu wakipigana ana imani gani kuhusu amani na utangamano: hakui akiona thamani yake.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 8 Kiswahili questions from this test