naQonda

CBC Grade 8 Kiswahili Opener Exam Term 3 2026 · Question 8

Kati ya haya, ni lipi lisiloathiriwa na mazingira?

From Kiswahili — Term 3 Opener Assessment 2026 (Set 11) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu wa Makala

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali la 7 hadi la 12.

Mazingira ni jumla ya mambo yanayomzunguka binadamu. Ni mambo ambayo hutokea kuwa sehemu ya maisha ya mja kuanzia kwenye tabia, mienendo, imani, itikadi na hata afya. Wengi husema kuwa mazingira ni kiungo cha maisha.

Mtoto anapozaliwa katika mazingira yaliyojaa uhuni na uhalifu, huenda kikawa vigumu kumwelekeza mtoto kama huyu katika kutenda mema. Kumbuka amezoea kuwaona watu wakipigana, wakiumizana na kutoana damu. Je, ana imani gani kuhusu amani na utangamano?

Mazingira aidha yanaweza kuathiri utendaji kazi wa mtu. Mtu aliyelelewa katika mazingira ya ulevi hatafanya juhudi kubwa kuishi bila ya kuwa mraibu kwani dunia yake wakati wa ukuaji wake ilisheheni ulevi. Mtoto wa aina hii hujua kila aina ya matusi kwa kuwa mazingira yake yalijaa wenye vinywa vichafu kila wakati.

8. Kati ya haya, ni lipi lisiloathiriwa na mazingira?

  1. AHulka ya binadamu.
  2. BImani ya binadamu.
  3. CAfya ya binadamu.
  4. DUtamaduni wa binadamu.

Answer

D. Utamaduni wa binadamu.

Kifungu kinataja tabia (hulka), mienendo, imani, itikadi na afya; utamaduni hautajwi.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 8 Kiswahili questions from this test