naQonda

CBC Grade 8 Kiswahili Opener Exam Term 2 2025 · Question 7

Kilimo ni njia mojawapo ya kujiendeleza kiuchumi. Unadhani ni kwa nini vijana wanakipuuza kilimo? (alama 1)

From Kiswahili — Term 2 Opener Assessment 2025 (Set 10) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali la 5 hadi la 8.
Tatizo la ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana limefika viwango vya kuhuzunisha. Wengi wao ambao wamesoma hadi vyuo vikuu wamekata tama na kuingilia matumizi ya dawa za kulevya. Serikali imelaumiwa pakubwa kwa kushindwa kukabiliana na hali hii.
Ni kweli kuwa serikali inapaswa kuweka mikakati itakayowawezesha raia wake kujindeleza. Hata hivyo, hana kuwa mtu husoma ili aajiriwe tu ni ya kupotosha. Elimu inapaswa kutufumbua akili na macho yetu ili tuweze kufikiria na kuona nafasi za kujiendeleza hata pale ambapo wengine wanafikiria kuwa hapana matumaini.
Mathalani, vijana waliosoma wakipata mtaji, wanaweza kufanikiwa katika shughuli za kilimo kuliko wazee wao. Hii ni kwa sababu watatumia teknolojia ya kisasa kuongeza rutuba katika mashamba, kukabiliana na wadudu wanaoharibu mimea na kupanda mimea inayostahimili hali mbalimbali za anga.
Kilimo ni kazi yenye hadhi kama nyingine yoyote. Wanaobeza shughuli za zaraa ilhali kwao kuna ardhi ya kutosha hawafai kudai kwamba hakuna nafasi za ajira.

7. Kilimo ni njia mojawapo ya kujiendeleza kiuchumi. Unadhani ni kwa nini vijana wanakipuuza kilimo? (alama 1)

Answer

Wanakichukulia kuwa kazi duni isiyo na hadhi.

Wanaobeza zaraa.

Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.

Answer this test freeGet it marked: create a free account

More Grade 8 Kiswahili questions from this test