CBC Grade 8 Kiswahili Opener Exam Term 2 2025 · Question 6
Jukumu la serikali ni lipi? (alama 1)
From Kiswahili — Term 2 Opener Assessment 2025 (Set 10) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali la 5 hadi la 8.
Tatizo la ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana limefika viwango vya kuhuzunisha. Wengi wao ambao wamesoma hadi vyuo vikuu wamekata tama na kuingilia matumizi ya dawa za kulevya. Serikali imelaumiwa pakubwa kwa kushindwa kukabiliana na hali hii.
Ni kweli kuwa serikali inapaswa kuweka mikakati itakayowawezesha raia wake kujindeleza. Hata hivyo, hana kuwa mtu husoma ili aajiriwe tu ni ya kupotosha. Elimu inapaswa kutufumbua akili na macho yetu ili tuweze kufikiria na kuona nafasi za kujiendeleza hata pale ambapo wengine wanafikiria kuwa hapana matumaini.
Mathalani, vijana waliosoma wakipata mtaji, wanaweza kufanikiwa katika shughuli za kilimo kuliko wazee wao. Hii ni kwa sababu watatumia teknolojia ya kisasa kuongeza rutuba katika mashamba, kukabiliana na wadudu wanaoharibu mimea na kupanda mimea inayostahimili hali mbalimbali za anga.
Kilimo ni kazi yenye hadhi kama nyingine yoyote. Wanaobeza shughuli za zaraa ilhali kwao kuna ardhi ya kutosha hawafai kudai kwamba hakuna nafasi za ajira.
6. Jukumu la serikali ni lipi? (alama 1)
- AKuwapa vijana kazi
- BKukabiliana na maovu
- CKulinda maslahi ya raia wake
- DKuwapa watu wote wenye elimu nafasi bora
Answer
C. Kulinda maslahi ya raia wake
Serikali inapaswa kuweka mikakati ya kuwawezesha raia kujiendeleza.
More Grade 8 Kiswahili questions from this test
- Kilimo ni njia mojawapo ya kujiendeleza kiuchumi. Unadhani ni kwa nini vijana wanakipuuza kilimo? (alama 1)Question 7
- Kisawe cha neno kilimo ni zaraa. Kisawe cha neno hadhi ni (alama 1)Question 8
- Eleza habari kuu inayojadiliwa katika aya ya kwanza kwa sentensi moja. (alama 1)Question 9
- Kifungu kinasema, ‘si vigumu kwa mtu aliyeelimika kupata njia za kujipatia chakula, mahali pa kukaa na kile…Question 10
- Andika ujumbe uliokolezwa katika aya ya mwisho kwa sentensi moja. (alama 1)Question 11
- Andika mada inayofaa zaidi kwa kifungu hiki. (alama 1)Question 12