CBC Grade 8 Kiswahili Opener Exam Term 2 2025 · Question 11
Andika ujumbe uliokolezwa katika aya ya mwisho kwa sentensi moja. (alama 1)
From Kiswahili — Term 2 Opener Assessment 2025 (Set 10) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufupisho
Ufupisho
Soma kifungu hiki kisha ujibu swali la 9 hadi la 12.
Kulingana na sheria za kimataifa, kila mtoto hana budi kupelekwa shule anapofikia umri ufaao ili aweze kupata elimu itakayomnufaisha baadaye. Kwa mintaarafu hiyo, nchi nyingi zimehakikisha kuwa elimu ya msingi, aghalabu kuanzia viwango vya chekechea hadi Gredi ya kumi na mbili inapatikana bila malipo au kwa gharama ya chini sana.
Mtoto akipata elimu hunufaika kwa njia anuwai. Si vigumu kwa mtu aliyeelimika kupata njia za kujipatia chakula, mahali pa kukaa na kile atakachovaa. Ni nadra kumwona mtu kama huyo akigeuka ombaomba mjini wala kuwataabisha watu kwa kuwapora mali yao.
Wazazi wanashauriwa kuunga mkono kikamilifu juhudi za serikali. Wahakikishe kuwa watoto wao wana sare, vitabu, kalamu, rula na nyenzo nyingine zinazohitajika wakiwa shuleni. Nasi watoto tukifika shuleni tusiwe watu wa kulaza damu; siku zote tukumbuke kuwa ajizi ni nyumba ya njaa. Uvivu masomoni hautatusaidia kutimiza malengo yetu kwa vyovyote vile.
11. Andika ujumbe uliokolezwa katika aya ya mwisho kwa sentensi moja. (alama 1)
Answer
Wazazi wawasaidie watoto shuleni nao watoto wasome kwa bidii ili watimize malengo yao.
Aya ya mwisho.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 8 Kiswahili questions from this test
- Andika mada inayofaa zaidi kwa kifungu hiki. (alama 1)Question 12
- Chagua jibu sahihi kujaza pengo la 13.Question 13
- Chagua jibu sahihi kujaza pengo la 14.Question 14
- Chagua jibu sahihi kujaza pengo la 15.Question 15
- Chagua jibu sahihi kujaza pengo la 16.Question 16
- Chagua jibu sahihi kujaza pengo la 17.Question 17