CBC Grade 8 Kiswahili Opener Exam Term 2 2025 · Question 8
Kisawe cha neno kilimo ni zaraa. Kisawe cha neno hadhi ni (alama 1)
From Kiswahili — Term 2 Opener Assessment 2025 (Set 10) · 1 mark · Topic: Kusoma, Msamiati
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali la 5 hadi la 8.
Tatizo la ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana limefika viwango vya kuhuzunisha. Wengi wao ambao wamesoma hadi vyuo vikuu wamekata tama na kuingilia matumizi ya dawa za kulevya. Serikali imelaumiwa pakubwa kwa kushindwa kukabiliana na hali hii.
Ni kweli kuwa serikali inapaswa kuweka mikakati itakayowawezesha raia wake kujindeleza. Hata hivyo, hana kuwa mtu husoma ili aajiriwe tu ni ya kupotosha. Elimu inapaswa kutufumbua akili na macho yetu ili tuweze kufikiria na kuona nafasi za kujiendeleza hata pale ambapo wengine wanafikiria kuwa hapana matumaini.
Mathalani, vijana waliosoma wakipata mtaji, wanaweza kufanikiwa katika shughuli za kilimo kuliko wazee wao. Hii ni kwa sababu watatumia teknolojia ya kisasa kuongeza rutuba katika mashamba, kukabiliana na wadudu wanaoharibu mimea na kupanda mimea inayostahimili hali mbalimbali za anga.
Kilimo ni kazi yenye hadhi kama nyingine yoyote. Wanaobeza shughuli za zaraa ilhali kwao kuna ardhi ya kutosha hawafai kudai kwamba hakuna nafasi za ajira.
8. Kisawe cha neno kilimo ni zaraa. Kisawe cha neno hadhi ni (alama 1)
- AHali
- BKazi
- CStaha
- DUkwasi
Answer
C. Staha
Hadhi ni heshima / staha.
More Grade 8 Kiswahili questions from this test
- Eleza habari kuu inayojadiliwa katika aya ya kwanza kwa sentensi moja. (alama 1)Question 9
- Kifungu kinasema, ‘si vigumu kwa mtu aliyeelimika kupata njia za kujipatia chakula, mahali pa kukaa na kile…Question 10
- Andika ujumbe uliokolezwa katika aya ya mwisho kwa sentensi moja. (alama 1)Question 11
- Andika mada inayofaa zaidi kwa kifungu hiki. (alama 1)Question 12
- Chagua jibu sahihi kujaza pengo la 13.Question 13
- Chagua jibu sahihi kujaza pengo la 14.Question 14