CBC Grade 8 Kiswahili Opener Exam Term 2 2025 · Question 4
Ni funzo lipi linalojitokeza katika kifungu hiki? (alama 1)
From Kiswahili — Term 2 Opener Assessment 2025 (Set 10) · 1 mark · Topic: Kusoma, Ufahamu
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali la 1 hadi 4.
Hapo zamani za kale, wanyama walikuwa na uwezo wa kufikiria na kuwasiliana kama afanyavyo binadamu. Mathalani, wale walao nyama walikutana mara kwa mara kubuni mikakati bora zaidi ya kuimarisha uwindaji wao. Wale walao nyasi nao walifahamishana kuhusu yalikopatikana malisho bora zaidi ili wahamie huko.
Siku moja, Kifaru, kiongozi wa wanyama katika nchi ya Tujueni, aliitisha mkutano wa wanyama wenzake walao mimea. Mkutano wenyewe uliazimia kujadili usalama wao. Wanyama wengi, wakubwa kwa wadogo walifika bila kuchelewa. Mkutanoni walikuwemo Sungura, Paa, Swara, Tohe, Ngiri, Mbogo, Tembo na Twiga.
Masuala mengi yaliangaziwa katika mkutano huo. Iligunduliwa kuwa wengi wao walijipata hatarini kutokana na kupuuza methali isemayo umoja ni nguvu utengano ni udhaifu. Kikao hicho kilipitisha mambo kadhaa. Ilipendekezwa wanyama wawe wakila katika makundi ili wasaidiane katika kujihami na kumtambua adui ajapo. Wale wakubwa kama Ndovu, Kiboko na Mbogo waliombwa wawawekee ulinzi wenzao wadogo wadogo. Wanyama walikula yamini kulindiana maslahi.
Walipokuwa wakifumukana, wanyama hao walimwona chui akiwavizia kwa karibu. Ndovu walitimua mbio kumkabili Chui kwa ghadhabu. Ama kweli hodi ya kifo haisubiriwi. Chui alifyatuka arubii kwa kasi ya umeme kuinusuru roho yake. Huku akitweta, aliwatahadharisha wenzake dhidi ya kuwavamia wanyama wale wakiwa katika makundi.
4. Ni funzo lipi linalojitokeza katika kifungu hiki? (alama 1)
Answer
Umoja ni nguvu – tushirikiane ili tujilinde.
Methali iliyotajwa.
Written answers can be worded differently: naQonda marks your own answer and explains it when you sign up free.
More Grade 8 Kiswahili questions from this test
- Nini kinasababisha wengine kuingilia matumizi ya dawa za kulevya kulingana na kifungu? (alama 1)Question 5
- Jukumu la serikali ni lipi? (alama 1)Question 6
- Kilimo ni njia mojawapo ya kujiendeleza kiuchumi. Unadhani ni kwa nini vijana wanakipuuza kilimo? (alama 1)Question 7
- Kisawe cha neno kilimo ni zaraa. Kisawe cha neno hadhi ni (alama 1)Question 8
- Eleza habari kuu inayojadiliwa katika aya ya kwanza kwa sentensi moja. (alama 1)Question 9
- Kifungu kinasema, ‘si vigumu kwa mtu aliyeelimika kupata njia za kujipatia chakula, mahali pa kukaa na kile…Question 10